JE BOCCO ANAONYESHA KUWA YEYE NI KIONGOZI KWELI?
Wakati anatua akitokea Azam fc John Bocco alionekana kama vile atashindwa kuwika , akataka kupambana kuwaonyesha watu hasa waajiri wake wa zamani kuwa anaweza kupambana kwenye hali zote.
Akapewa unahodha msaidizi kuanza maisha ndani ya simba ambapo siku za mwanzoni alianza vizuri baadaye akapata majeraha, akashuka kidogo. Hivi sasa amerudi kwenye kiwango chake na amekuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo hasa katika ufungaji kipindi hiki ambacho Emmanuel Okwi ni majeruhi.
Bocco amekuwa akipambana kila anapopewa nafasi ya kucheza na amedhihirisha kuwa yeye ni kiongozi kutokana na sasa kuwa kiongozi kamili baada ya kuondoka kwa Method Mwanjale, amekuwa akiwahamasisha wenzake uwanjanni zaidi.
Ikumbukwe mechi yao ya mwisho ya ligi ambayo simba ilishinda mabao 2 kwa sufuri [2-0] dhidi ya ndada yote yalifungwa na BOCCO.
Hivyo ni dhahiri anautumia uongozi wake vizuri na molali yake inaweza kumbeba kocha wake Djuma Masoud.
Comments
Post a Comment