MSHAHARA WA KOCHA MPYA SIMBA NI SHIDA. Alipwa 42,000 kwa dalika


Na Godfrey Mpagike.

Inawezekana akawa ndiye kocha aliyewahi kulipwa mshahara mkubwa zaidi Ligi Tanzania bara. Ni baada ya mshahara wake kupigiwa mahesabu na kugundua kuwa analipwa kiasi cha Tsh 42, 000 kwa dakika.

Kutokana na mshahara huo kocha huyo anatakiwa kuleta mabadiliko ya hali ya juu, ndani ya klabu ikiwa ni pamoja kumalizia kiporo cha ligi kuu Vpl vizuri ili aweze kutwaa ubingwa na pia kufanya vizuri pia kwenye michuano ya Kombe la shilikisho Afrika.

Ikumbukwe simba anaugulia maumivu tayari ya kutolewa kwenye mashindano ya FA ambayo Simba ndiye aliyekuwa bingwa mtetezi. Hivyo Simba analazimika kuchukua ubingwa Vpl ili mwakani apate tena nafasi ya kucheza Mechi za kimataifa Afrika la sihivyo achukue ubingwa shirikisho ili apite moja kwa moja.

Kwahiyo kwa taswira ya haraka kocha huyo Mfaransa anatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha simba inafanya vizuri hapo mbeleni, yasije mkuta ya Omog ndani ya klabu hiyo yenye jeuri ya fedha.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya