Mbaroni Kwa Kutapeli Milioni 15 za Raisi


Mbaroni Kwa Kutapeli Milioni 15 za Raisi
Kijana mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamedy Msangi (28) mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa jambo hilo na kusema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa na askari walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya kosa hilo kwa kuomba mkopo katika taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana. 

Matei amedai kuwa kijana huyo alipoomba mkopo huo aliorodhesha majina ya vijana wengine wanne akijifanya kuwa vijana hao wamejiunga kwenye kikundi hicho kisha kupatiwa mkopo huku hao vijana aliowaorodhesha wakiwa hana taarifa yoyote. 
Mbali na hilo Kamanda Matei alitoa rai kwa wananchi wa Morogoro na kuwataka wananchi kuacha wizi "Tuache huu wizi kwa kutumia vyombo vinavyotoa mikopo kwani mikopo hii imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa chini na hilo ndiyo lengo la Serikali kuwaondolea watu umasikini ili waweze kufungua viwanda vidogo vidogo na kujipatia kipato, lakini wapo watu wanatumia vibaya vikundi hivi" alisema  Matei

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya