Posts
Showing posts from January, 2018
NECTA Watangaza Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama
- Get link
- X
- Other Apps
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba. Jumla ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06. Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09. Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu. "Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde. Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika kara...
Mzee Majuto Akosa Kitanda Muhimbili Arudishwa Nyumbani
- Get link
- X
- Other Apps
Taarifa iliyoripotiwa January 25, 2018 ni kuhusu King Majuto ambapo ilisemakana kuwa amelazwa Muhimbili, sasa Masoud aliyetoa taarifa hiyo ambaye ni Afisa habari wa Chama cha Waigizaji ameelezea kuhusu Majuto kukosa kitanda Muhimbili na kurudishwa nyumbani. Masoud amesema kuwa kwa sasa Majuto anaishi Vingunguti kwa ndugu zake ila January 26, 2018 anaripoti hospitali kwa ajili ya vipimo na kinachomsumbua kikubwa ni Presha kwani mwili wake ulikuwa umechoka sana na bado Madaktari wanampima ilikujua tatizo kubwa ni nini.? "Mzee wetu majuto anaumwa na anaumwa kwa muda mrefu tulifanya utaratibu wa kutoka kwakwe kuja dar ili kutibiwa muhimbili alitakiwa kulazwa ila tukapewa taarifa na madaktari kuwa vitanda vimejaa tukarudi saa nane usiku" Masoud Jumanne ndo majibu yatatolewa kipi kinachomsumbua kwakuwa amepimwa mambo mengi
Kamanda Muslim Kushuhudia Mtanange wa Azam na Yanga Kesho
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya soka ya Azam FC imemtangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunatus Muslim, kuwa ndiye mgeni rasmi kwenye mchezo wake wa kesho dhidi ya Yanga. Akiongea leo mbele ya waandishi wa habari msemaji wa klabu hiyo Jaffary Idd amemtaja Kamanda Muslim kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ambao utawashuhudia mabingwa watetezi Yanga wakicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Azam Complex. Aidha Jaffary pia amesema pamoja na kuandika barua ya kuomba kubadilishwa kwa mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mchezo huo Israel Nkongo, lakini hadi sasa bado wanamtambua kama mwamuzi kwani hawajapata taarifa yoyote ya kukubaliwa au kukataliwa kwa ombi lao. Bado tunamtambua Israel Nkongo kama mwamuzi wa mchezo wetu wa kesho lakini tunamuomba atende haki'', amesema Jafarry. Kwa upande wake kocha msaidizi wa mabingwa hao wa mapinduzi Idd Cheche, amesema wanaiheshimu klabu ya Yanga lakini wamejiandaa kuhakikisha wanawapa raha na ladha ya soka mashabiki wa soka w...
Yanga Kuwakosa wachezaji hawa Mchezo wa Kesho Dhidi ya Azam FC
- Get link
- X
- Other Apps
Wachezaji saba wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wataukosa mchezo wa kesho unaotarajiwa kuchezwa dhidi ya Azam FC katika dimba la Azam Complex kutokana na sababu mbalimbali walizokuwa nazo. Hayo yamebainishwa leo na Afisa Habari wa klabu hiyo Dismas Ten na kuwataja wachezaji kuwa ni Yohana Mkomola, Thaban Kamusoko, Amisi Tambwe, Abdallah Shaibu, Donald Ngoma pamoja na Patongonyani ambao wote hawa ni majeruhi huku Pius Buswita akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. "Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC ni wachezaji saba pekee ndio watakaokosa mchezo huo kama nilivyosema lakini kila kitu kimekamilika. Tunaiheshimu sana Azam kwani wamekuwa na msimu mzuri wanapata matokeo ndani na nje ya uwanja wao wa nyumbani ila ata sisi Yanga SC tupo vizuri na tunatarajia kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho", alisema Dismas Ten. Azam FC kesho itakuwa inamkaribisha Yanga SC katika dimba lao la nyumbani...
SIMBA yazidi kujiweka pazuri baada ya kuifumua Kagera Sugar bao 2-0
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya soka ya Simba imelipa kisasi dhidi ya Kagera Sugar baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo uliomalizika jioni hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Simba ilibidi kusubiri hadi dakika ya 69 kuweza kupata bao lake la kwanza kupitia kwa kiungo Said Ndemla ambaye alipata pasi kutoka kwa Shiza Kichuya dakika 10 baadaye Simba kupitia kwa John Bocco wakaandika bao la pili. Matokeo ya leo yanaifanya Simba SC kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikifikisha alama 32 katika michezo 14 na kuishusha Azam FC yenye alama 30. Katika mchezo mwingine uliopigwa leo kati ya Singida United dhidi ya Majimaji FC, timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1 hivyo Singida kubakia katika nafasi ya 5 ikiwa na alama 24, nyuma ya Yanga na Mtibwa Sugar zenye alama 25. Msimu uliopita April 22, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar na kukwamishwa mipango yake ya ubingwa
NYOSSO mikononi mwa Polisi baada ya kumpiga shabiki mpaka kuzimia.
- Get link
- X
- Other Apps
Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limethibitisha kumshikilia mlinzi wa Kagera Sugar Juma Said Nyosso kwa kosa la kumpiga shabiki anayeaminika kuwa ni wa Simba baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa mjini Bukoba. Tukio hilo limetokea baada ya mechi kumalizika na wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo na mashabiki wakawa wanashangilia kwa kutoa maneno makali kitendo ambacho kilimfanya Nyosso akose uvumilivu na kumpiga shabiki huyo. Baada ya kupigwa ngumi shabiki huyo alianguka chini na kuonekana kama amepoteza fahamu ndipo Polisi walifika na kumkamata Nyosso na kuondoka naye. Aidha shabiki huyo alichukuliwa na gari ya wagonjwa na kumkimbiza hospitali kwaajili ya kupata huduma zaidi ikiwemo matibabu. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Augustine Orom amesema bado wanaendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo na wakikamilisha watatoa taarifa kamili.
Lazaro Mambosasa Akamea Trafiki Wanao Onea Wenye Vyombo vya Moto Baada ya Kuwakamata
- Get link
- X
- Other Apps
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa atoa maelezo ya wa jinsi Askari wa Usalama Barabarani(Trafiki), wanavyotakiwa kutekeleza majukumu yao. Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa Trafiki wamekuwa na tabia ya kusimamisha gari, kuomba leseni na kukagua kama dereva au mmliki wa gari ana vitu kama stika ya bima, taa, magurudumu, mtungi wa gesi ya kuzimia moto na viakisi mwanga(Reflector). Akafafanua kuwa Askari akisimamisha gari ni lazima akueleza sababu za kukusimamisha. Pia ni lazima aeleze anataka kukagua nini katika gari lako Akaongeza kuwa Trafiki wanatakiwa kutumia busara kumtoza faini Dereva ambaye gari lake lina matatizo ya taa kwa kuwa huenda hatumii gari hilo nyakati za usiku. Ufafanuzi huu umekuja wakati ambapo watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakilalamikia vitendo wanavyoviita vya kionezi kutoka kwa Askari wa Usalama Barabarani pamoja na kutozwa faini kubwa kwa makosa madogo
Binti mwenye uvimbe begani afariki dunia....Waziri Ummy Amlilia
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema amesikitishwa na kifo cha msichana Marim Sandalu (17) aliyekuwa na uvimbe begani. Mariam ambaye ni mkazi wa Masasi mkoani Mtwara, amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI). Binti huyo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji Muhimbili mwaka mmoja uliopita wakati huo uvimbe ukiwa bado mdogo, alitoweka baada ya kwenda katika tiba za asili kabla ya kurejea hospitalini hapo Januari 3 mwaka huu, baadaye kuhamishiwa katika taasisi hiyo. Waziri Ummy amesema inasikitisha kwani msaada wa Watanzania haukuweza kuokoa maisha yake. “Tutaongeza jitihada zaidi kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwahi hospitalini kufanyiwa uchunguzi na kuzingatia maelekezo ya madaktari wanayopewa ikiwamo kuanza matibabu mara moja na si kwenda kukaa nyumbani na mgonjwa,” amesema Waziri Ummy ambaye hivi karibuni alimtembelea Mariam hospitalini kumjulia hali.
Zitto Kabwe aweka wazi uwekezaji mzito Kigoma
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe amesema amepatikana mwekezaji wa kujenga maduka makubwa la biashara (malls) mkoani humo kama yale ya Mlimani City ya jijini Dar es Salaam. Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Community Center, Mwanga jana Januari 20, 2018, Zitto amesema haiwezekani mkoa wa Kigoma ukaendelea kubaki nyuma kimaendeleo. Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo amesema inapofika jioni mji wa Kigoma unakuwa kimya jambo alilodai kuwa haliwezi kuleta mabadiliko na kukuza mzunguko wa fedha. “Tumepata mwekezaji wa kujenga mall kubwa kama ya Mlimani City ili ikifika usiku kuwe kumechangamka. Hatuwezi kuendelea kuwa mkoa au mji wa mwisho,” amesema Zitto na kuongeza, “Haina maana sisi watoto wenu kusomeshwa na kuuacha mji huu ukaendelea kuwa hivi. Tunahangaika, mtuache tufanye kazi na mwaka 2020 mtaniuliza kupitia kile nilichoahidi na mtaninyonga kwa nilichowaahidi.” Kuhusu mapato ya halmashauri ...
Waziri Mpina awasilisha majina ya Viongozi waliokaidi agizo la Serikali
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewasilisha majina ya viongozi wa halmashauri ambazo hazijaanza kutekeleza upigaji chapa mifugo na zile ambazo ziko chini ya asilimia 10 ya utekelezaji, Kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ili zichukuliwe hatua. Mpina alibainisha hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa upigaji chapa mifugo nchini, mjini Dodoma. Alisema kwa tathmini iliyofanyika hadi sasa jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 wamepigwa chapa huku asilimia 40.7 wakiwa hawajapigwa chapa na zoezi hilo linatarajiwa kukamilishwa Januari 31, mwaka huu. “Halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 na Halmashauri 9 hazijaanza kupiga chapa,” alisema Mpina. Alizitaja halmashauri ambazo hazijaanza kabisa ni Tandahimba, Nanyum...
Waziri MWAKYEMBE AMCHANGIA WASTARA.
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe jana Januari 20, 2018 amemtembelea na kumjulia hali msanii wa filamu Wastara nyumbani kwake Tabata Sanene, Dar es Salaam. Wastara kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu na yupo kwenye maandalizi ya safari kwenda India kwa matibabu zaidi. Waziri Mwakyembe akiambatana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu na Katibu Mtendaji wa BASATA alimtakia kheri Wastara na kumkabidhi mchango wa Shs. 1,000,000/= (milioni moja). Aidha, Mwakyembe aliwasihi wasanii na Watanzania kwa ujumla kumchangia Wastara kwa hali na mali ili aweze kupata fedha za kumwezesha kwenda India kwa matibabu zaidi
JOHARI AFUNGUKA SIRI YA KIFO CHA MAMA YAKE
- Get link
- X
- Other Apps
MREMBO wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameanika siri ya kifo cha mama yake kwa kueleza namna ambavyo alipigana kutetea kifo cha mama yake mzazi. Johari alipata pigo hilo usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Hindu Mandali, jijini Dar es Salaam baada ya mama yake kulazwa kwa ugonjwa wa kisukari kwa saa chache tangu afikishwe hospitalini hapo. Kabla ya kupatwa na umauti huo, Johari alikuwa akiishi na mama yake mzazi, maeneo ya Gereji, Mabibo jijini Dar ambapo kwa zaidi ya miaka mitatu, msanii huyo alihangaika kutetea uhai wa mama yake, kwa nyakati tofauti. Katika kipindi chote hicho, Johari alikuwa mzito sana kuelezea mateso aliyokuwa anayapitia mama yake, zaidi alikuwa akiwaelezea watu wake wa karibu sana. Akizungumza na Risasi Jumamosi, akiwa kwenye nyumba ya familia, Mburahati jijini Dar, Johari alisema kifo cha mama yake kimekuwa pigo kubwa kwake na kueleza namna alivyopambana kumpigania. “Nimehangaika jamani. Nilikuwa silali, mchana na usiku nilik...
YANGA YAMKINGIA KIFUA BEKI WAKE MKONGOMAN. Yatoa sababu kwanini hayupo mpaka sasa.
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya soka ya Yanga imetoa sababu kwanini mlinzi wake mpya wa kimataifa Fiston 'Festo' Kayembe Kanku ameshindwa kujiunga na timu tangu asajiliwe Disemba 2017. Akiongea leo Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussein Nyika amesema mchezaji huyo raia wa DR Congo hajajiunga na timu kwasababu anashughulikia matatizo ya kifamilia. “Kanku ana matatizo makubwa ya kifamilia ndiyo maana tumempa ruhusa ya kwenda kuyashughulikia, akimaliza atakuja kuanza kazi, na atacheza tu ligi bado ina mechi nyingi sana,”amesema Nyika. Kwa upande mwingine Nyika ameongelea suala la uhamisho wa kimataifa (ITC), amabapo ameeleza kuwa ulikuwa unasumbua ila kwasasa wapo kwenye hatua za mwisho kuupata japo kuwa tayari mchezaji huyo ni mali ya Yanga. Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara wanashika nafasi ya 5 kwenye msimamo wakiwa na alama 22 kwenye mechi 13 walizocheza huku kesho wakishuka dimbani kucheza na Ruvu Shooting.
WAZUNGU WASHINDWA KUMUONDOA NDEMLA SIMBA.
- Get link
- X
- Other Apps
KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, sasa anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwepo Msimbazi huku ikielezwa lile dili la kwenda kucheza Ulaya limeyeyuka. Ndemla ambaye mkataba wake wa sasa na Simba unamalizika Aprili, mwaka huu, mwishoni mwa mwaka jana alikwenda Sweden kufanya majaribio kwenye timu ya AFC Eskelistuna na kufuzu. Hata hivyo, licha ya kufuzu majaribio hayo, Ndemla ameshindwa kujiunga na timu hiyo. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, uongozi umeridhishwa na kiwango cha Ndemla, hivyo wameona bora waendelee kuwa naye ili kukiongezea nguvu kikosi katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika. “Mkataba wake unaelekea ukingoni lakini wakati wowote anaweza kuongezewa kwa sababu uongozi unaridhishwa na kiwango chake ukizingatia kwamba tuna michuano ya kimataifa. “Hii inamaanisha kuwa, huu si wakati wa kuacha wachezaji kama yeye,” kilisema chanzo hicho. Alipotafutwa meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo kuzungumzia mustakabali wa Ndemla, alisema: ...
OBREY CHIRWA sasa ruksa kucheza dhidi ya Azam Fc. Raundi ya 15.
- Get link
- X
- Other Apps
Ni baada ya kumaliza adhabu yake ya mechi tatu kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha kwenye mechi dhidi ya Prisons. Mchezaji huyu atakwenda kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting itakayopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni ilikukamilisha adhabu yake. Chirwa ataendelea mkufanya mazoezi na wachezaji wenzake ili kunifua kwaajili ya mechi dhidi ya Azam fc utakao kamilisha raundi ya 15,kabla ya ligi kusimama kwa muda kabla ya mzunguko wa pili kuanza tena. Ikumbukwe Chirwa ameshaikosa michezo miwili tayari, ya Mbao fc na Mwadui fc. Hivyo Chirwa nae huenda akajumuishwa kwenye kikosi kitakacho vaana na Azam fc, mechi ambayo itapigwa katika dimba la azam comlex, Chamazi.