WACHEZAJI WETU WANA HASIRA SANA SINGIDA UNITED KUWENI MAKINI.


Baada ya kukaa nje kwa karibu nusu msimu kutokana na majeruhi, wachezaji Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko wamerejea kwenye kikosi cha Yanga kikamilifu.


Alianza kurejea Tambwe akaumia, akafuata Kamusoko na sasa Tambwe na Ngoma wamerejea kikamilifu tayari kuisaidia Yanga kutwaa taji la ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa nne, kutwaa kombe la FA pamoja na kutinga makundi kombe la Shirikisho.

Wachezaji hao tayari wameanza mazoezi na kikosi cha Yanga huku pia wakifanya mazoezi ya ziada ya Gym ili kuhakikisha wanakuwa 'fiti' kuhimili mikiki mikiki ya michuano yote.

Yanga iko kambini mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA (ASFC) dhidi ya Singida United unaotarajiwa kupigwa siku ya pasaka, April 01.

Kurejea kwa watatu hao ni habari njema sana kwa kikosi cha Yanga kuelekea mchezo huo kwani sasa Singida United itakumbana na Yanga iliyokamilika kwelikweli.

Yanga na Singida United tayari zimekutana mara tatu msimu huu. Zilikutana mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Zikakutana tena kwenye mzunguuko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Namfua na timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana.

Lakini pia zikakutana kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi na matokeo yakawa sare ya bao 1-1.

Katika michezo miwili ya mwisho, Yanga ilicheza bila idadi kubwa ya wachezaji muhimu ambao walikuwa majeruhi.

Tambwe, Kamusoko na Ngoma hawakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichopivaa Singida United katika michezo hiyo.

Lakini sasa watakuwa na nafasi ya kucheza dhidi ya walima alizeti hao ambao wananolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van Pluijm.

Pia mchezo huo wa robo fainali kombe la FA utakuwa wa aina yake kwani Yanga itaingia ikiwa katika kiwango bora zaidi msimu huu.

Baada ya kuanza msimu kwa kusuasua, Yanga sasa imechanganya kwani imeshinda michezo tisa mfululizo ya ligi wakati hali ikiwa tofauti kwa Singida United ambayo ilianza msimu kwa nguvu lakini inaonekana kupoteza makali yake kadiri msimu unavyoelekea ukingoni.

Mchezo huo lazima apatikane mshindi ambaye atatinga nusu fainali ya kombe la FA (ASFC) ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Baada ya mchezo huo, April 07 Yanga itashuka kwenye dimba la Taifa kuivaa Welayta Dicha kwenye mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho.

April 11 kwa mara nyingine, Yanga itaikaribisha Singida United kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.

Huu utakuwa moja ya michezo ambayo itatoa tathmini ya ubingwa kwa kikosi cha Yanga msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).