Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaosumbua watu wengi sana duniani. Mara nyhingi huanza kipindi cha balehe na huweza kuendelea mpaka mtu akiwa mtu mzima. Hujulikana kama pimpleskwa kiingereza au Acne Vulgaris kwa kitaalamu. Mara nyingi chunusi huanza katika wastani wa umri wa miaka 15 na huisha kabisa kwenye miaka 25, kwa baadhi ya watu chunusi huweza kuendelea mpaka miaka ya 40.
Chunusi huathiri uso, kifua au mgongo na hivyo huweza kusababisha mtu kukosa kujiamini, kukosa raha kutokana na muonekano wa sura yake kuathiriwa.
Ingawa huu ni ugonjwa kama mengine, watu wengi hawatafuti matibabau rasmi ya tatizo hili na hivyo wakati mwingine kusababisha tatizo kukua au kutotibiwa vizuri.

Namna Chunusi Zinavyotokea



Chunusi ni ugonjwa unaotokea katika njia ya vinyweleo vya ngozi. Kwa kawaida njia ya kinyweleo huwa na tezi za mafuta(sebum) ambayo huzalishwa kulainisha ngozi. Mafuta haya hupita kwenye njia ya kinyweleo mpaka kufika juu kwenye ngozi.
Chunusi zinapotokea huwa kuna: mafuta yanazalishwa kwa wingi zaidi, bakteria kuingia kwenye njia ya kinyweleo na hatimaye kuziba kwa njia ya kinyweleo.
Chunusi hutokea kutokana vitu vikuu vitatu. Kwanza, ngozi kutoa mafuta mengi. Pili, bakteria kushambulia njia za vinyweleo. Tatu, njia za vinyweleo kuziba.
Ngozi ina tezi za mafuta ambayo kazi yake ni kulainisha ngozi. Kutokana na mabadiliko ya homoni wakati wa balehe, mafuta haya huzalishwa kwa wingi zaidi ya kawaida. Mafuta haya hujaa kwenye njia za vinyweleo.
Bakteria aina ya Propionibacterium acneswanaokaa kwenye njia za vinyweleo hushambulia mafuta haya na kutengeneza kemikali za muwako wa ngozi. Bakteria huongezeka na seli nyingine za mwili hulundikana.
Hatimaye njia za vinyweleo huziba. Hivyo mlundikano wa mafuta, bakteria na seli za mwili zilizokufa huvimba na kutengeneza vipele vya chunusi.

Sababu Za Chunusi Kutokea



Sababu kuu ya chunusi kutokea ni mabadiliko ya homoni. Kwa wengi ni kipindi cha balehe ambapo homoni za aina ya androgen huongezeka mwili na hivyo kusababisha mafuta ya ngozi(sebum) kuongezeka.
Sababu nyingine ni:
  • Magonjwa kama Polycystic ovary syndrome na congenital adrenal hyperplasia.

Dalili


Mara nyingi chunusi hujitokeza katika umri wa balehe na kuacha kwenye miaka 25 au mapema ya hapo. Kwa baadhi ya watu, chunusi huendelea zaidi ya hapo ambapo huweza kuleta athari zaidi kwenye ngozi.
Zinapoanza, chunusi huleta vipele vya ukubwa tofauti kwenye uso. Mara nyingi sana huanza usoni kisha zinaweza kutokea sehemu nyingine za mwili kama mabega, mgongoni na sehemu ya juu ya kifua.
Ngozi inaweza kuwa inang’aa sana kutokana na kuwa na mafuta mengi.
Vipele vya chunusi huanza kwa ukubwa tofauti, vingine vikiwa vidogo na vingine vikubwa. Vinaweza kuwa na usaha, na baada ya kupasuka na kupona mara nyingi huacha madoti meusi.
Chunusi hutofautiana katika ya mtu na mtu, na nyakati tofauti kwa mtu mmoja. Zinaweza kuwa kidogo, vingi kidogo au vingi sana.

Matibabu



Matibabu ya chunusi hutegemea na ukali wa ugonjwa huu. Njia za matibabu huhusisha dawa za kupaka kwenye ngozi au dawa za kunywa. Chunusi za ukali mdogo na wastani dawa za kupaka peke yake zinaweza kutumika wakati chunusi kali mchanganyiko wa dawa za kupaka na kunywa hutumika.
Matibabu ya chunusi yanaweza kuchukua muda mrefu, wakati mwingine miezi 3 mpaka 6 au zaidi kutegemea na ukali. Hivyo uvumilivu na kufuata maelekezo na matumizi ya dawa ni muhimu ili kutibu tatizo hili.
Dawa Za Kupaka


Dawa za Retinoids
Dawa za retinoids huingia kwenye njia ya kinyweleo na kuzuia utokeaji wa vipele vipya. Pia husaidia kupunguza mabaka hasa kwa watu wenye ngozi nyeusi. Dawa hii hupakwa sehemu za ngozi zilizothiriwa na chunusi. Chunusii zenye ukali mdogo, dawa hii pekee huweza kutosha kwa matibabu. Ikiwa chunusi ni nyingi sana, basi dawa zingine huweza kuongezwa. Baadhi ya dawa za retinoid za kupaka ni Tazarotene, Tretinoin na Adapalene. Kupata matokeo mazuri zaidi na dawa hizi, inashauriwa kutumia mpaka wiki 12 (miezi 3). Ishu kubwa kwa dawa za retinoids ni irritation ya ngozi.
Dawa Za Kuua Bakteria Za Kupaka(topical antibiotoics)
Utokeaji wa chunusi huchangiwa na bakteria aina ya Propionibacterium acnes. Hivyo njia nyingine ya matibabau ni kutumia dawa za kuua bakteria huyu. Dawa za kuua bakteria za kupaka kama Benzoyl peroxide, Clindamycin na ErythromycinClindamycin naErythromycin hufanya kazi vizuri zaidi inapotumiwa na Benzoyl peroxide au dawa za Retinoids.
Dawa Za Kunywa

Dawa Za Kuua Bakteria
Dawa za kuua bakteria (antibiotics)hutumika kutibu chunusi kali zinazohusisha uso, mgongo, kifua na mabega. Dawa hizi huua bakteria wanaochangia kuleta chunusi. Dawa kama Tetracycline, Doxycycline, Minocycline, and Trimethoprim–sulfamethoxazole (Septrin) hutumika kutibu chunusi. Ufanisi wa dawa hizi katika kutibu chunusi huanza kuangaliwa baada ya wiki 6, kama maendeleo hayaridhishi basi unaweza kubadilishiwa dawa. Matibabu yanaweza kwenda hadi miezi 3 ili kupata matokeo mazuri.
Dawa Za Homoni
Pale ambapo inaonekana chunusi kwa wanawake zinachangiwa na homoni basi dawa za homoni huweza kutumika kutibu tatizo hili. Dawa hizi zinaweza kujumuisha vidonge vya uzazi wa mpango, spinorolactone na dawa zingine.
Dawa ya Isotretinoin
Watu wenye chunusi kali sana ambazo hazijakubali matibabu ya dawa za kunywa na kupaka zinaweza kutibiwa kwa isotretinoin. Dawa hii hupunguza uzalishwaji wa mafuta kwenye ngozi na kuzuia bakteria kuzaliana hivyo kudhibiti chunusi. Inaweza kutumika kwa miezi kadhaa katika kutibu chunusi. Kwa wanawake wanaotumia dawa hii ni lazima watumie njia za kuzuia mimba kwani iwapo atashika mimba dawa hii huathiri maumbile ya mtoto (birth defects).
Baada ya chunusi kuisha, unaweza kuwekwa kwenye dawa angalau kwa miezi 2 ili kuzuia kujirudia. Baadhi ya wagonjwa huitaji kuwekwa kwenye dawa za kupaka kwa muda mrefu ili kuzuia chunusi kujirudia.
Ni muhimu kabla ya kutumia dawa hizi uonane na daktari kwa uchunguzi, vipimo na ushauri. Dawa hizi huathiri mimba, hivyo muhimu kumweleza daktari wako kama ni una mimba au unatarajia kupata ujauzito kipindi utakachokuwa kwenye matibabu

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).