MACHO YOTE KWA YANGA SASA. By Kotei.

Kiraka wa Simba, James Kotei amedai vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara sasa imenoga na mchezo wao ujao dhidi ya Yanga utakuwa wa kukata na shoka.
Kotei alisema tofauti na awali, sasa Ligi Kuu imekuwa moto kutokana na ushindani mkubwa ulioletwa na Yanga.
Simba sasa inaongoza Ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa kwani inalingana pointi 46 na Yanga iliyopo nafasi ya pili. Hata hivyo Simba ina mchezo mmoja mkononi.
"Ligi imekuwa ngumu sasa, ni tofauti na mwanzo. Hata hivyo hii ndiyo inaongeza utamu wa Ligi," alisema Kotei.
"Mechi yetu ijayo ni dhidi ya Yanga, itakuwa ngumu. Uzuri ni kwamba sisi hatuna mechi za FA hivyo tuna muda wa kutosha kujiandaa," alisema Kotei.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).