SINGIDA UNITED YAJIBU MAPIGO YA YANGA.


Klabu ya soka ya Singida United imejibu mapigo ya maandalizi ya mchezo wake wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwa kuweka kambi mbali na dimba lao la Namfua mkoani Singida.

Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa kikosi hicho kimeondoka katikati ya mji wa Singida na kuelekea pembezoni mwa Mkoa huo kwaajili ya kujiandaa kuelekea mchezo huo utakaopigwa April 1, 2018.

Wakati Singida wakifanya hivyo mabingwa wa soka nchini Yanga, nao wameondoka jijini Dar es salaam jana kuelekea mkoani Morogoro ambako itaweka kambi kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Kambi za Singida United na Yanga zote zinawakosa wachezaji wao ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa ambayo leo inashuka dimbani kucheza na DR Congo kwenye mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA.

Singida United inamkosa nahodha wake Mudathir Yahya wakati Yanga inawakosa Ibrahim Ajib, Kelvin Yondani, Hassan Kessy, Gadiel Michael na Ramadhani Kabwili. Wachezaji hao watajiunga na timu zao baada ya mchezo wa leo

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).