HABARI MPYA KUHUSU DONALD NGOMA na HAMIS TAMBWE.

Image result for DONALD NGOMA NA AMIS TAMBWE
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao walikuwa majeruhi watajiunga kikosini Alhamisi Yanga itakapoanza maandalizi ya kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Ten amesema baada ya kikosi cha Yanga kurejea kutoka Botswana, wachezaji walipewa mapumziko ya siku kadhaa na wanatarajia kuanza kambi keshokutwa Alhamisi.

"Kwa sasa hatuna wachezaji majeruhi. Amissi Tambwe na Donald Ngoma wamekuwa wakifanya mazoezi peke yao, Alhamisi watajiunga na wenzao"

Yanga itashuka dimbani April 02, 2018 katika uwanja wa Namfua kuikabili Singida United kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA.

Bofya hapa kuona video hii




TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI NDUGU MSOMAJI

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).