Simba Yamtangaza HARUNA NIYONZIMA

Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Afisa habari wake Haji Manara wamethibitisha kumsajili kiungo mwenye uraia wa Rwanda Haruna Niyonzima kuwatumuika wanamsimbazi hao. 

Hayo yameweka wazi leo na Manara wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika kumbi za mikutano za 'New Millenium Tower' eneo la Makumbusho Jijini Dar es Salaam na kusema Niyonzima ni mmoja wa wachezaji ambao watashiriki katika mchezo wao wa kwanza wa 'Simba Day' Agosti nane. 

"Kuna mambo anayashughulikia huko Kigali akimaliza atakuja inaweza akaja na timu au kabla ila atacheza katika mechi ya ufunguzi Simba day. tarehe 8 kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo U -20 ya Simba itacheza na timu ambayo itatangazwa kesho, 'maveteran' wa Simba pia 

watacheza,Simba Queens watacheza) wapinzani wao pia kutajwa kesho. Pia siku hiyo kutaanzishwa zawadi kwa wachezaji bora zaidi wa msimu ambapo tutamtangaza  mchezaji wa zamani aliyechezea simba kwa mafanikio makubwa.", amesema Manara. 

Pamoja na hayo, Manara amesema wanatarajia kuipokea timu yao mnamo Agosti 5 kutokea nchini Afrika Kusini ilipokwenda kuweka kambi maalum ya kujifua kuelekea msimu mpya ligi kuu unaotarajiwa kuanza siku si nyingi kutokea sasa.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya