KUMBE HARMONIZE ANAPENDA KUSIKILIZA WIMBO HUU WA ALI KIBA

Msanii wa Bongo Flava, Harmonize amesema anapenda kusikiliza nyimbo za wasanii mbali mbali akiwemo Alikiba. 

Muimbaji huyo anafanya kazi chini ya label ya WCB ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz ambaye imekuwa ikivumishwa kutoelewana na Alikiba. 

“Zamani sana nilikuwa nasikiliza nyimbo za Ali, nafikiri ilikuwa Mac Muga  kama sikosei, Mac Muga nilikuwa nasikiliza sana, so… hivyo!,” amesema Harmonize katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm. 

Awali alitangulia kusema kuwa huwa anapenda kusikiliza ngoma za wasanii wengi sana hususani wa Tanzania kwa sababu anaamini akiwasikiliza wasanii wenzake anajifunza vitu vingi. 

“Siyo Ali pekee yake kuna nyimbo za wasanii wengi nasikilizaga, namsikilizaga Barnaba na wasanii wengine waimbaji wa WCB na nje ya WCB pia,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya