Kiungo mpya wa Yanga mtambo wa MABAO

Kiungo mpya wa timu hiyo, Raphael Daud kutoka Mbeya City.
YANGA imelamba dume baada ya kukamilisha usajili wa kiungo mpya wa timu hiyo, Raphael Daud kutoka Mbeya City kwani rekodi zake zinaonyesha ni mtambo wa mabao kwa kuwa ni mtengenezaji pamoja na mfungaji mzuri. Yanga imekamilisha dili la kumsajili kiungo huyo na kumpatia mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo kurithi nafasi ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyetimkia Simba.

Takwimu za Raphael aliyepandishwa Mbeya kutoka kikosi B cha timu msimu wa 2014/15 ni kuwa msimu uliopita ambao Yanga walibeba ubingwa alipitwa na mfungaji bora, Simon Msuva kwa idadi ya mabao sita pekee baada ya Msuva kufunga 14 huku yeye akifunga nane.
Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi.
Kuonyesha kwamba ingawa ni kiungo mchezeshaji ambaye kazi yake ni kuwatengenezea nafasi za kufunga lakini yeye anaweza kuwatungua makipa pia kwenye msimu wa 2015/16 alifanikiwa kucheka na nyavu mara sita. Pia Raphael kwenye msimu wa 2014/15 akiwa na Mbeya City alifanikiwa kurudi kambani mara nne, jambo ambalo linamfanya kwa muda wote aliokaa Mbeya City na kuichezea mechi 64 ameifungia mabao 18 yanayomfanya awe mfungaji bora wa muda wote ndani ya kikosi hicho.

Wanamfuatia kwa kufunga Mbeya City ni Patrick Mwakanguku mwenye 17, Mwegane Yeya aliyefunga 12, Paul Nonga mwenye 10 ba Deus Kaseke aliyefunga mabao tisa. Wachezaji hao sasa wote hawapo na Mbeya City ambapo Kaseke yupo Singida United, Nonga yupo Mwadui na Yeya yeye alishaachana na soka. Kwa takwimu hizo inaonyesha Yanga hawajapata hasara ya kumpoteza Niyonzima kwani Raphael ana uwezo wa kuifanya kazi aliyokuwa anaifanya pamoja na uwezo wa kufunga ambapo atasaidiana na washambuliaji wa timu hiyo

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya