Posts

Showing posts from August, 2017

LEO KAMA JANA AU LAA. Tshishimbi kung'ara tena au laa

Image
Leo ni leo pia ambapo mabingwa watetezi YANGA watakuwa uwanjani, kuwavaa Wana wa Paluhengo LIPULI FC kutoka IRINGA huku yanga wakiwa na kiu kubwa tena mara baada ya kupewa kiu na watani wao wa jadi hapo Jana SIMBA mara baada ya kuwacharaza vilivyo RUVU katika uwanja wa Taifa.   Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa mnamo majira ya saa 10 jioni kulingana na ratiba, hivyo tupende kuwataarifu wapenzi wasomaji na watazamaji wa soka kuwa leo tutakuwa tukiwaletea matokeo yote live, kwa kutumia video za magoli nakadharika.  Dont miss it  By Godfrey Mpagike 

VIDEO: The best dancer in the world

Image

YANGA YAZIDI KUJIIMARISHA. Hatimaye Kiungo mpya asaini miaka Mwili

Image
HATIMAYE  kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), leo amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wa Tanzania, Yanga SC.  Mchezaji huyo alikuwa nchini wiki iliyopita kwa ajili ya vipimo vya afya na baada ya kufaulu akaambiwa afuate barua ya kuruhusiwa na klabu yake, Mbabane Swallows ya Swaziland kuondoka ili aje kusaini mkataba.  Baada ya kukamilisha taratibu hizo, Tshishimbi leo amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika mabao ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.  Na baada ya kusaini mkataba huo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye inaaminika ndiye mrithi wa Mnyarwanda, Haruna Niyonzima aliyekwenda kwa mahasimu Simba, anatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda kisiwani Pemba kuungana na kikosi cha Yanga kwa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Agosti 23.  Yanga ilivutiwa na Tshishimbi baada ya kumuona akiichezea ...

Msuva azidi kuwa vizuri (mechi 4 magoli 6)

Image
WINGA  wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefikisha mabao sita ya kufunga tangu amejiunga na Difaa Hassani El-Jadida (DHJ) ya Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola.  Hiyo inafuatia Msuva jana kufunga bao moja katika mechi yake nane DHJ ikifungwa 2-1 na timu ya Daraja la Kwanza, Union Sportive Musulmane Oujda (USMO) Uwanja wa El Abdi mjini Jadida.  “Jana nimefunga tena, hilo ni bao langu la sita sasa katika mechi nane zote za kirafiki. Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na hapa kila siku ninachojua ni bidii tu ili nitimize malengo yangu,”amesema Msuva akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo.  Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na DHJ Julai 28, mwaka huu baada ya kucheza  Yanga ya nyumbani, Tanzania tangu mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro.  Awali ya hapo, Msuva alipitia akademi ya Azam akitokea kituo cha kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi, Wakat...

NIYONZIMA awapa YANGA siri hii

Image
KIUNGO mpya wa kimataifa wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amewafichulia wapinzani wao wote wa Ligi Kuu Bara mambo ya ndani kuhusu kiwango chao akiwataka kujipanga vilivyo kuelekea ligi hiyo hapo Agosti 26, mwaka huu.  Akizungumza na gazeti hili jana, Niyonzima alisema kiwango walichoonyesha katika mechi dhidi ya Rayon ni sehemu ndogo ya "ufundi" walionao wachezaji wa timu hiyo ambao msimu ujao wamejipanga kuipa klabu yao mataji. Kiungo huyo aliyetua Simba hivi karibuni kwa kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, alisema kila mchezaji aliyesajiliwa Simba anafahamu kiu ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambao wamekosa ubingwa kwa miaka minne.  Niyonzima alisema kuwa kwa sasa wanaendelea kujifua na kabla ligi haijaanza, watakuwa wameimarika zaidi kwa sababu wachezaji wote wamekamilika na wanafanya mazoezi ya pamoja.  "Tutakuwa wazuri zaidi ligi itakapoanza, tulionyesha kiasi kidogo tu cha uwezo wetu, naamini masha...

MBILI KALI ZA YANGA LEO

Image
YANGA LEO  JUMAMOSI 12.8.2017 Mchezo wa Kirafiki Klabu ya Yanga Leo inatarajiwa Kushuka Dimbani Kucheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Chamazi katika Hali ya Kujiandaa na Ligi KUU Tanzania Bara na Mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Simba. Mchezo huo awali  ndugu mwana kwataunit.com ulikuwa uchezwe Taifa Ila Jana ulihamishiwa Chamazi Baada ya Yanga kupewa Taarifa kutoka Serikalini Kutoutumia uwanja huo. Yanga Itawakosa wachezaji wanne Yanga katika Mchezo wa Leo dhidi ya Ruvu itawakosa wachezaji Youthe Rostand, Beno Kakolanya, Mwashiuya na Obrey Chirwa wachezaji hawa wote ni majeruhi japo ndugu msomaji wa GODYNEWSTZ  hali zao zinaelezwa kuwa siyo mbaya sana. Kwamujibu wa Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema Afya zao zinaendelea Vizuri na wote wataungana kambi ya Pemba kujiandaa na Ligi na Mechi dhidi ya Simba

HUJACHELEWA MAGAZETI YA LEO 12/08/2017 HAYA HAPA

Image

KUMBE HARMONIZE ANAPENDA KUSIKILIZA WIMBO HUU WA ALI KIBA

Image
Msanii wa Bongo Flava, Harmonize amesema anapenda kusikiliza nyimbo za wasanii mbali mbali akiwemo Alikiba.  Muimbaji huyo anafanya kazi chini ya label ya WCB ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz ambaye imekuwa ikivumishwa kutoelewana na Alikiba.  “Zamani sana nilikuwa nasikiliza nyimbo za Ali, nafikiri ilikuwa Mac Muga  kama sikosei, Mac Muga nilikuwa nasikiliza sana, so… hivyo!,” amesema Harmonize katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm.  Awali alitangulia kusema kuwa huwa anapenda kusikiliza ngoma za wasanii wengi sana hususani wa Tanzania kwa sababu anaamini akiwasikiliza wasanii wenzake anajifunza vitu vingi.  “Siyo Ali pekee yake kuna nyimbo za wasanii wengi nasikilizaga, namsikilizaga Barnaba na wasanii wengine waimbaji wa WCB na nje ya WCB pia,” amesema.

HII NDIYO HABARI YA MJINI KUHUSU KOMBE LA DUNIA

Image
Shirikisho la Soka la Morocco limetangaza kwamba litawasilisha ombi la kutaka kuwa mwenyekiti wa Kombe la Dunia la 2026. Siku ya mwisho kwa nchi kuwasilisha nia ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ni leo Ijumaa, na baadaye Fifa itathibitisha nchi ambazo zimewasilisha maombi. Marekani, Canada na Mexico zilitangaza mwezi Aprili kwamba zitawasilisha ombi la kuwa wenyeji kwa pamoja. Ni taifa moja pekee ambalo limewahi kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia barani Afrika - Afrika Kusini mwaka 2010 - na hii itakuwa mara ya tano kwa Morocco kutaka kuwa mwenyeji. Shirikisho la Soka Afrika (Caf) liliunga mkono juhudi za Morocco mwezi Julai. Jumla ya timu 48, badala ya 32 ilivyo sasa, zitashiriki katika michuano hiyo mwaka 2026 baada ya timu kuongezwa kwenye mabadiliko yaliyotangazwa na Fifa mapema mwaka huu. Uamuzi wa nani mwenyeji utafanyawa mwaka 2020. Sera ya Fifa ya mzunguko ina maana kwamba Afrika ni moja ya mashirikisho ambayo yanaweza kuwasilisha maombi ya kuwa mwen...

MNIGERIA WA YANGA NI SHIDA

Image
KATIKA kuiimarisha safu yao ya ulinzi, Yanga imemshusha nchini beki Mnigeria, Eisa Mfowoshe aliyemaliza mkataba wa kuichezea Klabu ya Itihad ya Oman. Ujio wa beki huyo unakamilisha idadi ya wachezaji watatu waliokuwepo kwenye majaribio ya timu hiyo wengine ni beki Mnigeria, Henry Okoh na kiungo Fernando Bongyang na Mfowoshe. Kati ya wachezaji hao mmoja pekee ndiye anatakiwa asajiliwe ili akamilishe idadi ya wachezaji saba wa kimataifa kati ya sita ambao tayari wamesajiliwa na Yanga. Championi Ijumaa lilikuwepo kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kumshuhudia beki huyo akionyesha uzoefu wa kupambana na washambuliaji wenye uwezo wa juu. Katika mazoezi hayo, beki huyo mwenye umbile kubwa alionekana akifanya program zote kwa makini huku akionyesha uhodari wake wa kupiga pasi zilizonyooka ndefu na fupi kwa wenzake. Wakati mazoezi hayo yakiendelea, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina alimpangia washambuliaji wawili, Donald Ngo...

HAYA NDIYO YALIYOJILI BAADA YA SIMBA DAY. hapo jana

Image
Ni mara baada ya hapo jana Simba (mnyama) kuwatambulisha wachezaji wake wapya. Baadhi ya mashabiki wamekuwa na maoni mbalimbali japo kuwa wengi wao wamejawa na furaha wakiamini kuwa huu ndio mwaka wa Simba kufanya kweli na kuonyesha kufarijika baada ya kukosa ubingwa kwa muda mrefu zaidi. Akiongea na GodynewsTz shabiki mmoja alisikika akisema sasa kwa simba hii nilazima tuchukue nasi ubongwa mara tatu mfululizo kama sio mara nne.  Tusubirie hapo ligi itakapo Anza mana hatuwezi kujaji kwa mechi hizi chache. Haya ndio maneno ya baadhi ya watani wa jadi.  By Godfrey Mpagike  The super Skeleton boy 

Kiungo mpya wa Yanga mtambo wa MABAO

Image
Kiungo mpya wa timu hiyo, Raphael Daud kutoka Mbeya City. YANGA imelamba dume baada ya kukamilisha usajili wa kiungo mpya wa timu hiyo, Raphael Daud kutoka Mbeya City kwani rekodi zake zinaonyesha ni mtambo wa mabao kwa kuwa ni mtengenezaji pamoja na mfungaji mzuri. Yanga imekamilisha dili la kumsajili kiungo huyo na kumpatia mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo kurithi nafasi ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyetimkia Simba. Takwimu za Raphael aliyepandishwa Mbeya kutoka kikosi B cha timu msimu wa 2014/15 ni kuwa msimu uliopita ambao Yanga walibeba ubingwa alipitwa na mfungaji bora, Simon Msuva kwa idadi ya mabao sita pekee baada ya Msuva kufunga 14 huku yeye akifunga nane. Wachezaji wa Yanga wakiendelea na mazoezi. Kuonyesha kwamba ingawa ni kiungo mchezeshaji ambaye kazi yake ni kuwatengenezea nafasi za kufunga lakini yeye anaweza kuwatungua makipa pia kwenye msimu wa 2015/16 alifanikiwa kucheka na nyavu mara sita. Pia Raphael kwenye msimu wa 2014/15 akiw...

Ujumbe wa MESSI kwa NEYMAR Jr

Image
Kuondoka kwa Neymar katika klabu ya soka ya Barcelona kunaweza kukawa kumemuumiza zaidi Lionel Messi ambaye amekuwa karibu zaidi na mchezaji huyo kwa takribani misimu minne. Messi kupitia mtandao wa Instagram, amemuandikia ujumbe wa kumuaga rafiki yake huyo ambaye anatarajiwa kukamilisha usajili wake wa kujiunga na PSG ya Ufaransa wiki hii kwa ada ya uhamisho utakaovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 198. “It was a great pleasure to have shared all these years with you, friend @neymarjr. I wish you good luck in this new stage of your life. See you tomorrow,” ameandika Messi katika mtandao huo. Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 akitokea Santos ya nchini kwao Brazil

Manara :TUTACHEZESHA WACHEZAJI TISA DHIDI YA YANGA

Image
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports Club, Haji Sunday Manara aiomba Shirikisho la soka nchini (TFF) iwaruhusu kuchezesha wachezaji tisa uwanjani badala ya 11 katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga SC. Manara ameyasemahayo huku akitanabaisha kuwa kipigo chao kwa Yanga hakiepukiki. “Mchezo wa Yanga na Simba natamani uwekesho kwa sababu inasaidia kupunguza kelele mtaani na maneno ya kuzuazua”. “Tunawaomba TFF kama wataweza waturuhusu tuanze na wachezaji tisa hivi kama wataturuhusu na kanuni zinaruhusu tutawaandikia barua rasmi ikiwezekana tuanze tisa tutawafunga tu Yanga” Afisa huyo aliyetoka kifungoni hivi karibuni kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameongeza kuwa ameyapokea kwa mikono miwili maamuzi ya Kocha Mkuu wa Simba Omog juu ya kumvua unahodha, Jonas Mkude “Mimi ukiniambia, kwangu nimefurahia hili kwa sababu ukiwa nahodha unakuwa unabeba vichwa vya wachezaji kumi sasa kutolewa katika unahodha itamsaidi...

CHUJI AIBUKIA NDANDA GC

Image
ATHUMAN IDDI ‘CHUJI’. KIUNGO wa zamani wa klabu ya Yanga, Simba na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Athuman Iddi ‘Chuji’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara.  Awali Chuji ilisemekana anataka kujiunga na Mbeya City, lakini nyota huyo jana alithibitisha kujiunga na Ndanda kwa mkataba huo wa mwaka mmoja.  Akizungumza na Nipashe jana, Chuji alisema jana asubuhi alikuwa akitegemea kuelekea Mtwara kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu.  “Ni kweli, jana nimekutana na viongozi wa timu hiyo wakiwa na makocha na nimesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Ndanda,” alisema Chuji.  Aidha, alisema kwa sasa anajipanga kuhakikisha anaisaidia timu hiyo msimu ujao ili iweze kufanya vizuri.  “Tumepanga kuondoka leo asubuhi hii (jana) kuelekea Mtwara kuungana na wenzangu ambao tayari wapo kwenye maandalizi,” aliongezea kusema Chuji.  Hata hivyo, kusajiliwa kwa nyota huyo kumeleta utata katika kuthib...