NIYONZIMA. YANGA ni lazima wakalie kichapo.

KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ameweka wazi kuwa anaamini klabu yake itapata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wao, Yanga licha ya yeye kutokuwepo katika kikosi cha timu hiyo kutokana na kupata msiba wa dada yake nchini kwao.

Niyonzima alisafiri usiku wa juzi Jumatano kwa ajili ya kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya kuwahi msiba wa dada yake ambapo ataukosa mchezo huo wa Simba dhidi ya Yanga ambao utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kwenye mchezo wa kwanza ambao kiungo huyo alikuwepo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Mechi iliyopigwa Oktoba 28, mwaka jana katika Dimba la Uhuru.

Akizungumza na Championi Ijumaa, kiungo huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ alisema kuwa mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi juu ya kutokuwepo kwake kwa sababu anawaamini wachezaji wenzake watapata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo ya Kariakoo Dabi.

“Mashabiki wao wanatakiwa kutuliza roho zao kwani licha ya mimi kutokuwepo katika mchezo huu lakini Simba ina kikosi kipana na wachezaji waliobaki wanaweza kuifanya kazi ya kupata matokeo mazuri mbele ya wenzetu na pia ninawaombea,” alisema.

Mauno feni ya MANGE KIMAMBI.
INDE ya DULLY
BOFYA HAPA UJIONEE

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).