HAT-TRICK YA MESSI YAWEKA REKODI


Nyota wa Barcelona Lionel Messi usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kufunga mabao matatu (hat-trick) akiisaidia timu yake ya Barcelona kuifikia rekodi ya kucheza mechi 38 mfululizo bila kupoteza.

Messi amefunga mabao hayo dhidi ya Leganes ambapo sasa timu hiyo imecheza mechi 38 za La Liga bila kupoteza ikifikia rekodi ya Real Sociadad ya kucheza mechi 38 bila kupoteza ambapo ilifanya hivyo misimu ya 1978-79 na 1979-80.

Bao la kwanza la Messi lilipatikana kwa njia ya mkwaju wa adhabu ndogo (Freekick) nje kidogo ya eneo la 18 ambapo sasa amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao akiwa nje ya 18 katika mechi 6 mfululizo tangu msimu wa 2003/04.

Barcelona ambayo ina alama 79 kileleni mwa msimamo wa La Liga huenda ikaweka rekodi ya kuwa timu ambayo haijapoteza mechi nyingi zaidi endapo itashinda mchezo wake ujao dhidi ya Valencia

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).