MZEE AKILI MALI APIGA DUA NZITO KULEKEA MTANANGE WA WATANI WA JADI.


Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amesema kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya watani zao Simba SC kunahaja ya kutupilia mbali tofauti zao na kumuomba Mungu katika kuhakikisha wanachomoza na ushindi siku hiyo ya Aprili 29.

Wakati zimesalia siku mbili pekee kabla ya kukutana kwa watani hao wajadi Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye dimba la Taifa siku ya Jumapili hii, Mzee Akilimali ametumia muda wake kuiyombea timu yake kuhakikisha inachomoza na ushindi siku hiyo.

Tunalengo la kuwashinda wapinzani wetu, siyo rahisi lakini lazima ujiandae kwa hayo wazee tunatoa baraka zote kwa vijana kwakuwa hatuna kinyongo.

Isipokuwa mimi naomba tu Yaarabbi Yaarabbi nakuomba turudishie hali yetu ileile ya umoja na mshikamano wetu kwa kila hali, tushikamane kwaajili ya kuwasapato vijana wetu na tumuombe Mwenyezi Mungu kila mmoja kwa dua yake na imani yake ili tupate ushindi siku hiyo ya Jumapili.

Nawaomba wana Yanga wenzangu tuwe wamoja tuwache tofauti zetu twende katika mchezo maana ni mgumu sana.

Kocha mpya ameingia na viongozi wetu wamefanya mambo haraka haraka sasa hivi yupo kazini, Msimbazi ubingwa bado isipokuwa tu mtu hawezi kukata tamaa ila hali bado. Amenitambuka mechi chache tu na yeye atarajie kufanya vibaya kwenye mechi hizo alizo nazo.

Wazee hatuna ahadi yoyote kwa vijana kwakuwa hayo yanatamkwa na viongozi.

Simba ambayo inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwakuwa na jumla ya pointi 59 nyuma ya hasimu wake Yanga wenye alama 48 zinatarajia kukutana siku ya Jumapili ya Aprili 29 kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es salaam

Mange kimambi afunguka haya baada ya watanzania kutoandamana
Bofya hapa,share ,pia usisahau kusubscribe

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).