Posts

Showing posts from April, 2018

NGOMA AJUTIA MAAMUZI YAKE NDANI YA YANGA.

Image
Ishu ya Donald Ngoma kupitia kwa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, ameandika machache kuhusiana na mchezaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Donald Ngoma, ambaye hajaonekana Uwanjani kwa muda mrefu. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Teni ameandika ujumbe akieleza kuwa maisha ni changamoto hivyo kuna wakati lazima uzipitie ili uweze kushinda. "Ndiyo maana yakaitwa maisha, kuna wakati ni lazima upitie changamoto ili kuyashindao Bofya hapa kuona goli la Simba 1 vs Yanga 0.

TUJUKUMBUSHE KIDOGO MATOKEO TOKA 1965 MPAKA 2017,Yanga aendelea kuongoza kwa matokeo na points.

Image
REKODI YA SIMBA NA YANGA LIGI KUU PEKEE P W D L Pts  Yanga SC 98 36 33 26 113 Simba SC 98 26 33 36 83 MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA ZA WATANI WA JADI; JUNI 7, 1965 Yanga v Sunderland (Simba) 1-0 MFUNGAJI: Mawazo Shomvi dk. 15). JUNI 3, 1966 Yanga v Sunderland (Simba) 3-2 WAFUNGAJI: Yanga: Abdulrahman Lukongo dk. 54, Andrew Tematema dk 67, Emmanuel Makaidi dk. 83. Sunderland: Mustafa Choteka dk 24, Haji Lesso dk. 86. NOVEMBA 26, 1966 Sunderland v Yanga 1-0 MFUNGAJI: Mustafa Choteka dk. 44. MACHI 30, 1968 Yanga v Sunderland 1-0 MFUNGAJI: Kitwana Manara dk. 28. JUNI 1, 1968 Yanga v Sunderland 5-0 WAFUNGAJI: Maulid Dilunga dk. 18 (penalti), Dilunga dk. 43, Salehe Zimbwe dk. 54, Zimbwe dk. 89, Kitwana Manara dk. 86. MACHI 3, 1969 Yanga v Sunderland (Yanga ilipewa pointi za chee na ushindi wa mabao 2-0, baada ya Sunderland kugoma kuingia uwanjani). JUNI 4, 1972 Yanga v Sunderland 1-1 WAFUNGAJI: Yanga: Kitwana Manara dk. 19, Sunderland: Willy Mwaijibe ...

ELASTO NYONI AWAGONGELEA MSUMARI WA KICHWA YANGA.

Image
Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo Aprili 29, 2018 jijini Dar es salaam. Goli la Simba limefungwa na Erasto Nyoni kunako dakika ya 37 kipindi cha Kwanza kwa makosa ya mabeki wa Yanga. Hata hivyo mchezo huo ulionekana kuwa sawa kwa timu zote mbili kwani timu hizo zilionekana kushambuliana kwa zamu. Kwa matokeo hayo Simba SC wameendelea kujiimarisha kileleni kwenye msimamo wa VPL kwa alama 62 wakifuatiwa na Azam alama 49 na huku Yanga wakisalia nafasi ya tatu kwa alama 48. Bofya hapa kutazama bao la simba vs Yanga 

Ali Kiba Agoma Katu Katu Kumwalika Diamond Kwenye Harusi yake Inayofanyikaka Dar Leo

Image
Licha ya habari kusema kuwa Diamond yupo tayari kuhudhuria sherehe ya harusi ya Alikiba Jioni Ya leo hii, lakini upande wa Diamond umesema hajaalikwa. Chanzo kilicho karibu na Alikiba kimeiambia GPL .... . “Kiba anaonekana bado hayuko poa na Diamond, kamfanyia mwenzake jambo la kushangaza sana maana huwezi amini hadi dakika hii hajamualika kwenye sherehe yake ya harusi, yaani inaonekana Kiba hayuko tayari kushirikiana na mwenzake maana mara nyingi amekuwa akijishusha lakini hampi ushirikiano,” . . Nae Aidan Seif ambaye ni meneja wa Alikiba alipoulizwa na GPL kuhusu issue hiyo amesema . “Hadi sasa hatujamualika na kwa kweli sijajua kama tutamualika,” . . Hata hivyo mastaa tofauti nchini wamealikwa. Tusubiri na tuone.

MBINU MPYA ALIYOIPATIA YANGA KOCHA MPYA

Image
KOCHA mpya wa Yanga, Mkongomani Zahera Mwinyi, ametuliza mizuka ya wachezaji kwa kuwataka wacheze mpira mwingi na wala wasiichukulie mechi ya leo kama kitu cha ajabu sana mpaka kufikia hatua ya kupaniki. Mwinyi ambaye anazungumza kiswahili chenye lafudhi ya Congo, amewaambia wachezaji kwamba suluhisho la kuifunga Simba ni kutawala mchezo kwa kuuchezea mpira mara nyingi kadri inavyowezekana. Kocha huyo alitoa maelekezo hayo kwa wachezaji kambini, na kuwasisitiza kwamba wasihofie ujio wake kwa vile hatabadilisha mambo mengi lakini atawaongezea uwezo zaidi kwa vile wote wako vizuri. “Kocha anaonekana yuko fiti sana na kama tutapata muda mzuri wa kuwa naye naamini tutatisha sana huko mbeleni, huwezi kuamini baada ya kuanza kutufundisha alituambia tucheze sana mpira kwani njia pekee ya ushindi ni kujituma kwa kucheza kwani ukiweza kumiliki mpira muda mrefu utakuwa na uhakika wa kupata matokeo mazuri kwa mpinzani wako yeyote,” alidokeza mchezaji mmoja nyota wa Yanga. “Anaonekana ni mtu wa ...

Simba na Yanga zatumia Milioni 11 Moro

Image
Kikosi cha timu ya Yanga. IMEBAINIKA kuwa, timu za Simba na Yanga, zote zimetumia zaidi ya Sh11 milioni kwa ajili ya kambi zao mkoani Morogoro zilipokuwa zikijiandaa na mchezo wao wa leo Jumapili wa Ligi Kuu Bara. Simba ambayo iliingia Morogoro Jumapili ya wiki iliyopita na kuondoka Alhamisi ya wiki hii, ilifikia kwenye Hoteli ya Moro View iliyopo maeneo ya Nanenane. Yanga ambayo nayo iliingia Morogoro Jumatatu ya wiki hii, iliondoka juzi Ijumaa huku ikiweka makazi yake kwenye Hoteli ya Kingsway iliyopo mitaa ya Msamvu. Simba ambayo ilikuwa na msafara wa watu wasiopungua 29. Kulala Moro View Hotel mtu mmoja Sh25,000 watu 29 ni Sh 725,000, kwa siku nne walizolala hapo ni sawa na Sh 2,900,000 kwa watu hao wote. Sehemu ya kufanyia mazoezi, Jumatatu Simba ilifanyia kwenye Uwanja wa Highland uliopo Bigwa ambapo gharama zake si chini ya Sh 150,000 kwa siku. Siku ya Jumanne, Jumatano na Alhamisi, Simba ilifanyia kwenye Uwanja wa Jamhuri ambapo kwa mujibu wa wasimamizi wa uwanja...

Yanga yawapa ilani waamuzi watakaochezesha Mechi ya leo dhidi ya Simba

Image
  Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka Waamuzi watakaochezesha mchezo wa leo dhidi ya Simba kufuata sheria 17 za mchezo wa soka. Kauli hiyo imetolewa na Yanga kupitia Afisa Habari wa timu hiyo, Dismas Teni, ambapo kikosi chao kitakuwa mgeni dhidi ya Simba. Teni ameeleza kuwa timu zimewekeza kwenye mpira hivyo haitopendeza kuona Waamuzi wanaharibu ladha ya mpira na kushindwa kutafsiri sheria 17 za mchezo wa soka. Timu hizo zinakutana kesho ikiwa ni katika mzunguko wa pili wa ligi, baada ya ule wa kwanza kwenda sare ya bao 1-1.

SERIKALI YA ZIMVABWE YAGAWA LESENI ZA KULIMA BANGI.

Image
Serikali ya Zimbabwe imetoa ruhusa kisheria bangi kulimwa kama zao jingine la chakula au biashara. Ruhusa hiyo imetolewa ili zao hilo litumike kwaajili ya sababu za matibabu. Kwa watakaotaka kulima zao hilo, watapewa leseni ya miaka mitano kwaajili ya kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi na bidhaa zake zilizokaushwa. Zimbabwe ndio nchi ya pili Afrika kufanya jambo hili baada ya Lesotho kuwa ya kwanza kugawa leseni za kufanya kilimo hicho mwezi September mwaka 2017.

NIYONZIMA. YANGA ni lazima wakalie kichapo.

Image
KIUNGO  mchezeshaji wa Simba, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ameweka wazi kuwa anaamini klabu yake itapata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wao, Yanga licha ya yeye kutokuwepo katika kikosi cha timu hiyo kutokana na kupata msiba wa dada yake nchini kwao. Niyonzima alisafiri usiku wa juzi Jumatano kwa ajili ya kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya kuwahi msiba wa dada yake ambapo ataukosa mchezo huo wa Simba dhidi ya Yanga ambao utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Kwenye mchezo wa kwanza ambao kiungo huyo alikuwepo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Mechi iliyopigwa Oktoba 28, mwaka jana katika Dimba la Uhuru. Akizungumza na Championi Ijumaa, kiungo huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ alisema kuwa mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi juu ya kutokuwepo kwake kwa sababu anawaamini wachezaji wenzake watapata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo ya Kariakoo Dabi. “Mashabiki wao wanatakiwa kutuliza roho zao kwani licha ya mimi kutokuwepo katika m...