UTABILI WA CANNAVARO MECHI NA MAJIMAJI

Huu Hapa Utabiri wa Canavaro kwa Yanga Kuelekea Mechi ya Kesho Dhidi ya Majimaji
Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amefunguka na kudai mechi yao ya kesho dhidi ya Majimaji FC itakuwa ngumu kutokana na hali ya kiwanja kutokuwa vizuri huku akiahidi watafanya kila wawezalo ili kutoka na pointi tatu.

Canavaro ameeleza hayo kupitia ukurasa wao maalum wa timu ikiwa imebaki siku ya leo tu, kushuka katika dimba la Majimaji lililopo mkoani Ruvuma katika mchezo wa ligi kuu mzunguko wa tatu.
"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufika salama Songea, lakini kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Majimaji naamini utakuwa mgumu sana kutokana na wapinzani wetu wamejiandaa vizuri ila kwa upande wetu tumejiandaa vizuri zaidi yao kwa sababu tunajua kila mechi ni fainali kwetu", amesema Canavaro.
Pamoja na hayo, Canavaro ameendelea kwa kusema "Japokuwa tunafahamu tutakutana katika mazingira magumu ikiwemo kiwanja siyo kizuri lakini kwetu sisi ushindi ni muhimu ili tuweze kupata pointi 3 na tuweze kurejea nyumbani tukiwa na jumla ya alama sita", amesisitiza Canavaro.

Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro'
Kwa upande mwingine, Canavaro amekiri kwamba ligi kuu ya safari hii imekuwa ngumu kwa kuwa kila timu imejipanga vizuri katika kusaka pointi tatu kila iingiapo uwanjani lakini kwa niaba ya timu yake ameahidi watatetea ubingwa wao ili kikombe kizidi kubaki Jangwani

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya