HABARI NJEMA KWA WANA YANGA

Winga machachari wa klabu ya Yanga, Emmanuel Martin anatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ndanda siku ya Jumamosi kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.
Martin aliumia vibaya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Maji Maji wiki iliyopita hali iliyomfanya kupoteza fahamu kwenye dimba la Majimaji mjini Songea ambapo Yanga walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji wao hao.
Licha ya kuumia vibaya na kuzua hofu miongoni mwa wakereketwa wa klabu hiyo ya Yanga, Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu amethibitisha kuwa mchezaji huyo amerejea kwenye hali yake ya kawaida na ameendelea na mazoezi yake sambamba na wachezaji wenzake.
“Martin anaendelea vizuri na tayari ameanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya mchezo ujao na kama suala la kucheza mchezo huo litabaki kuwa chini ya kocha George Lwandamina lakini mchezaji yupo vizuri,” alisema Martin wakati akiongea na Mwanaspoti
Yanga wataumana na Ndanda kwenye mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya Vodacom wakiwa na alama zao tano kibindoni kutoka kwenye michezo mitatu ambayo wameshacheza mpaka sasa, wakitoa sare miwili na kushinda mmoja.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya