OKWI AZITAKA POINT TATU KWA YANGA

Mshambuliaji wa simba, Mganda, Emmanuel Okwi
KIUNGO mshambuliaji wa simba Mganda, Emmanuel Okwi, ametangaza kuwa kila mechi kwao ni fainali, hivyo watahakikisha wanapambana kushinda kila mechi itakayokuwa mbele yao ikiwemo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga.
Kauli hiyo, aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC na timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku mawili yakifungwa na Okwi na lingine John Bocco.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Oktoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza nasi, Okwi alisema malengo yake makubwa ni kushinda kila mechi mbele yao ili kuhakikisha wanajiwekea mazingira mazuri ya ubingwa kwenye msimu huu.
Kikosi cha timu ya Simba.
Okwi alisema, anaamini ushirikiano mkubwa anaoendelea kuupata kwa wachezaji wanzake, ndiyo umefanikisha yeye kufunga mabao sita kwenye mechi mbili, ambazo amezicheza huku akikosa mchezo mmoja pekee wa ligi kuu dhidi ya Azam FC.

Aliongeza kuwa, anawaomba mashabiki wa timu hiyo kuendelea kujitokeza uwanjani kwenye mechi za ligi kuu zikiwemo za mikoani kwa ajili ya kuwapa sapoti.
“Kila siku ninaendelea kumuomba Mungu niendelee kufunga idadi (kubwa) ya mabao ili kuisaidia timu yangu iweze kutwaa ubingwa wa ligi kuu tunaoupambania.

“Kikubwa tulichopanga pamoja na wachezaji wenzangu ni kushinda kila mechi ikiwemo dhidi ya Yanga ili tujiwekee mazingira ya ubingwa ambao ndiyo jambo la msingi.

“Na haya mabao ambayo ninaendelea kuyafunga sitakiwi kupata sifa mimi pekee, yametokana na ushirikiano mzuri wa wachezaji wenzangu katika kufanikisha timu inapata ushindi,” alisema Okwi

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya