SIMBA. Omog haondloki

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imesema kwamba ina imani kubwa na kocha wake, Mcameroon, Joseph Marius Omog na haina mpango wa kuachana naye kama inavyovumishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo mjini Tabora kwamba klabu haina mpango wa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kama inayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu aliowaita wasioitakia mema klabu hiyo.

“Nimekwishaeleza tangu awali kwamba, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumuondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo,”amesema Manara na kuongeza;
“Tunawaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka imani yao kwa uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo,” alisema Manara.

Omog yupo katika msimu wake wa pili, tangu ajiunge na Simba SC msimu uliopita kufuatia awali kuwahi kuifundisha klabu nyingine ya Tanzania, Azam FC.

Katika msimu wake wa kwanza tu ulioputa, Omog aliipa Simba taji la Azam Sports Federation Cup na kuiwezesha kurejea kwenye michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013, ikikata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Na katika msimu wake wa pili ambao amelenga kutwaa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambalo Simba ililibeba mara ya mwisho mwaka 2012, Omog amewaongoza Weekundu hao wa Msimbazi kuvuna pointi nane ndani ya mechi nne, wakishinda mechi mbili nyumbani na kutoa sare mbili zote za ugenini.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).