Msuva Mcgezaji bora wa mwezi.
SAIMONI MSUVA ATWAA TUZO YA MWEZI YA MCHEZAJI BORA
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Difaa al Jadida raia wa Tanzania Saimoni Msuva ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ya mwezi wa nane ndani ya klabu hiyo.
Msuva aliyejiunga na timu hiyo mapema mwezi wa nane baada ya kuuzwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC , aliingia katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo sambamba na mchezaji mwenzake kiungo mkabaji Said Mohamedi na Msuva kuibuka kidedea kwa kura 268 na mwenzake kupata kura 129. Kura hizo zinapigwa na wanachama wa klabu hiyo kama Simba SC wafanyavyo hapa nchini.
Msuva amefanikiwa katika hilo baada yakuwa msaada mkubwa kwenye timu hiyo kwa mwezi huo katika mechi za kirafiki akicheza mechi 13 na kufunga goli 9.
Huu ni mwanzo mzuri kwa kiungo huyo huko ughaibuni anasimama kama balozi mzuri wa soka la Tanzania. Licha ya kupata tuzo hiyo pia Msuva aliporudi nchini kwa ajili ya kuitumikia timu ya Taifa dhidi ya Botswana, alifunga goli mbili pekee za ushindi na kuiwezesha timu yake ya taifa kung'ara katika mchezo huo uliokuwepo katika kalenda ya FIFA.

Comments
Post a Comment