Posts

Showing posts from September, 2017

SIMBA. Omog haondloki

Image
KLABU  ya Simba ya Dar es Salaam imesema kwamba ina imani kubwa na kocha wake, Mcameroon, Joseph Marius Omog na haina mpango wa kuachana naye kama inavyovumishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo mjini Tabora kwamba klabu haina mpango wa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kama inayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu aliowaita wasioitakia mema klabu hiyo. “Nimekwishaeleza tangu awali kwamba, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumuondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo,”amesema Manara na kuongeza; “Tunawaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka imani yao kwa uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo,” alisema Manara. Omog yupo katika msimu wake wa pili, tangu ajiunge na Simba SC msimu uliopita kufuatia awali kuwahi kuifund...

VIDEO.Goli la kusawazisha la Mbao fc na Kotei leo 21st September 2017

Image
Nini unataka tena mtazamaji Usosahau KUSUSCRIBE hapo juu kupata habari mapema zaidi

VIDEO. Goli la kichuya

Image

Matokeo Mpaka sasa Mapumziko. Simba Vs Mbao

Mapumziko simba Vs mbao 1-0

AHADI YA MBAO KWA WANAMSIMBAZI LEO.

Image
Klabu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza imeahidi leo kuchukua ushindi dhidi ya Simba na kubeba pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaochezwa leo katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  Mbao FC ambao wao ni wenyeji wa mchezo wamejigamba kushinda mchezo huo kwa kutumia nafasi ya wenyeji wao kuigalagaza klabu ya Simba ambayo nayo imetinga jijini Mwanza toka mwanzoni mwa wiki kujiandaa dhidi ya Mbao FC.  "Siku ndio leo vijana wenu tunajitupa Uwanjani kuumana na Simba kwenye Ligi Kuu ya Vodacom. Jitokezeni kwa wingi CCM Kirumba kutupa hamasa vijana wenu ili kuhakikisha mnyama anakaa mapema. Mechi itakuwa ngumu lakini sisi ndio wenyeji kwa hiyo tuna kila sababu ya kushinda maana mcheza kwao hutunzwa"  Imesema taarifa ya Mbao FC  Klabu ya Mbao FC ni kati ya klabu ambayo iliipa shida Simba msimu uliopita katika mechi walizokutana ambapo Simba alishinda mechi hizo lakini ni kwa shida sana

LIVE MATOKEO YA Simba Vs Mbao leo.

Karibuni sana ndugu wasomaji wa blog yetu makini.  Jipatie matokeo ya mechi ya leo live kati ya simba na Mbao fc. 

OKWI AZITAKA POINT TATU KWA YANGA

Image
Mshambuliaji wa simba, Mganda, Emmanuel Okwi KIUNGO mshambuliaji wa simba  Mganda,   Emmanuel Okwi , ametangaza kuwa kila mechi kwao ni fainali, hivyo watahakikisha wanapambana kushinda kila mechi itakayokuwa mbele yao ikiwemo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga. Kauli hiyo, aliitoa mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC na timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku mawili yakifungwa na Okwi na lingine  John Bocco. Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Oktoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza nasi, Okwi alisema malengo yake makubwa ni kushinda kila mechi mbele yao ili kuhakikisha wanajiwekea mazingira mazuri ya ubingwa kwenye msimu huu. Kikosi cha timu ya Simba. Okwi alisema, anaamini ushirikiano mkubwa anaoendelea kuupata kwa wachezaji wanzake, ndiyo umefanikisha yeye kufunga mabao sita kwenye mechi mbili, ambazo amezicheza huku akikosa mchezo mmoja pekee wa ligi kuu dhidi ya Aza...

HABARI NJEMA KWA WANA YANGA

Image
Winga machachari wa klabu ya Yanga, Emmanuel Martin anatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ndanda siku ya Jumamosi kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam. Martin aliumia vibaya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Maji Maji wiki iliyopita hali iliyomfanya kupoteza fahamu kwenye dimba la Majimaji mjini Songea ambapo Yanga walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji wao hao. Licha ya kuumia vibaya na kuzua hofu miongoni mwa wakereketwa wa klabu hiyo ya Yanga, Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu amethibitisha kuwa mchezaji huyo amerejea kwenye hali yake ya kawaida na ameendelea na mazoezi yake sambamba na wachezaji wenzake. “Martin anaendelea vizuri na tayari ameanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya mchezo ujao na kama suala la kucheza mchezo huo litabaki kuwa chini ya kocha George Lwandamina lakini mchezaji yupo vizuri,” alisema Martin wakati akiongea na  Mwanaspoti Yanga wataumana na Ndanda kwenye mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ya Vodacom wakiwa...

Nani Mkali

Image
HARUNA NIYONZIMA vs TSHISHIMBI Kulikuwa na maneno mengi kabla ya ligi kuu Tanzania bara haijaanza. Hii ni kutokana na sajili mbalimbali zilizofanywa na vilabu mbalimbali. Nadhani mpaka sasa baada ya hizi mechi mbili ambazo kila timu imezicheza tinaweza tukawa angalau tuna namna ambayo tunaweza tukajaji mchezaji mmoja mmoja mfano NIYONZIMA NA TSHISHIMBI, Hii inakuja baada ya wachezaji hawa kuteka mabishano ya watu mara baada ya kusaini mikataba na timu zao mpya. Je ni nani ambaye mpaka sasa kati ya  hawa wawili nani ambye katisha mpaka sasa majibu unayo wewe. Na kiraka wetu.

Baada ya kuchoshwa na Bata ndogondogo za Diamond ZARI Afanya kufuru

Image
Zari Hassan Afanya Kufuru Kwa Pesa za Ivan..Achoshwa na Bata Ndogo Ndogo za Diamond Platnumz Katika hali ya kuonesha kukerwa na tabia ya diamond kutoka na mshiriki wa big brother 2013 dillish mathews zari amepost kwa page yake ya snapchat kuonesha kwamba hachoshwi na batavuzi ndogo ndogo na kuamua kununua gari mbili aina ya mercedes benz g 63 na bentley mulsane...Aanza Kumkubaka Marehemu Ivan Katika Posts zake

UTABILI WA CANNAVARO MECHI NA MAJIMAJI

Image
Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amefunguka na kudai mechi yao ya kesho dhidi ya Majimaji FC itakuwa ngumu kutokana na hali ya kiwanja kutokuwa vizuri huku akiahidi watafanya kila wawezalo ili kutoka na pointi tatu. Canavaro ameeleza hayo kupitia ukurasa wao maalum wa timu ikiwa imebaki siku ya leo tu, kushuka katika dimba la Majimaji lililopo mkoani Ruvuma katika mchezo wa ligi kuu mzunguko wa tatu. "Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufika salama Songea, lakini kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Majimaji naamini utakuwa mgumu sana kutokana na wapinzani wetu wamejiandaa vizuri ila kwa upande wetu tumejiandaa vizuri zaidi yao kwa sababu tunajua kila mechi ni fainali kwetu", amesema Canavaro. Pamoja na hayo, Canavaro ameendelea kwa kusema "Japokuwa tunafahamu tutakutana katika mazingira magumu ikiwemo kiwanja siyo kizuri lakini kwetu sisi ushindi ni muhimu ili tuweze kupata pointi 3 na tuweze kurejea nyumbani tukiwa na jumla ya alama sita...

Msuva Mcgezaji bora wa mwezi.

SAIMONI MSUVA ATWAA TUZO YA MWEZI YA MCHEZAJI BORA Kiungo mshambuliaji wa timu ya Difaa al Jadida raia wa Tanzania Saimoni Msuva ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ya mwezi wa nane ndani ya klabu hiyo. Msuva aliyejiunga na timu hiyo mapema mwezi wa nane baada ya kuuzwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC , aliingia katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo sambamba na mchezaji mwenzake kiungo mkabaji Said Mohamedi na Msuva kuibuka kidedea kwa kura 268 na mwenzake kupata kura 129. Kura hizo zinapigwa na wanachama wa klabu hiyo kama Simba SC wafanyavyo hapa nchini. Msuva amefanikiwa katika hilo baada yakuwa msaada mkubwa kwenye timu hiyo kwa mwezi huo katika mechi za kirafiki akicheza mechi 13 na kufunga goli 9. Huu ni mwanzo mzuri kwa kiungo huyo huko ughaibuni anasimama kama balozi mzuri wa soka la Tanzania. Licha ya kupata tuzo hiyo pia Msuva aliporudi nchini kwa ajili ya kuitumikia timu ya Taifa dhidi ya Botswana, alifunga goli mbili pekee za ushindi na kuiwez...

HAJI MWINYI. Napambana na hali yangu

Image
BEKI wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi Mgwali, msimu uliopita ndiye aliyekuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilipokuwa kikipambana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Alicheza mechi nyingi sana kumshinda mbadala wake Oscar Joshua waliyekuwa wakibadilishana naye katika nafasi hiyo. Hali hiyo ilitokana na uhodari aliokuwa akiuonyesha uwanjani kumshinda mpinzani wake ambaye pia huko nyuma ndiye aliyekuwa tegemeo ndani ya timu hiyo. Hata hivyo, baada ya  hivi karibuni Yanga kumsajili beki mwingine wa kushoto, Gadiel Michael, aliyetokea Azam FC na kuamua kuachana na Joshua, mambo yanaonekana kuwa magumu kwa Mwinyi. Tangu Gadiel ajiunge na Yanga, kwa sasa yeye ndiye anayeokana kuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina. Lwandamina amekuwa akivutiwa zaidi na uwezo mkubwa wa Gadiel ambao anauonyesha uwanjani kuanzia mazoezini mpaka kwenye mechi. Kutokana na hali hiyo, Mwinyi ambaye msimu uliopita alikuwa ndiye chaguo la kwanza la makocha hao kia...

MUNGINE ASHAMBULIWA DAR KWA RISASI

Image
Ikiwa ni siku tano tu zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma, tukio lingine kama hilo limetokea Dar es Salaam ambapo watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali Vincent Mritaba. Tukio hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali Mritaba akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni. Hadi usiku wa jana Madaktari walikua wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine

ACNE VULGARIS (Chunusi)

Acne vulgaris  (or simply  acne ) is a common human skin disease, characterized by areas of seborrhea (scaly red skin), comedones (blackheads and whiteheads), papules (pinheads), nodules (large papules), pimples, and possibly scarring. Aside from scarring, its main effects are psychological, such as reduced self-esteem and in very extreme cases, depression or suicide. One study has estimated the incidence of suicidal ideation in patients with acne as 7.1%. In adolescence, acne is usually caused by an increase in androgens such as testosterone, which occurs during puberty, regardless of sex. Acne more often affects skin with a greater number of oil glands; these areas include the face, the upper part of the chest, and the back. Severe acne is inflammatory, but acne can also manifest in noninflammatory forms. The skin changes are caused by changes in pilosebaceous units, skin structures consisting of a hair follicle and its associated sebaceous gland, changes that require and...

TUNDU LISU APIGWA RISASI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu  baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma. Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amesema Mbowe  "Hali ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa" Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya. Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma. Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea. Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upa...

VIDEO. Goli la pili MSUVA dakika ya 62

Image
Goli la pili Taifasyars vs Botswana

Tanzania 2 Botswana 0.

Image
Dakika ya 62 Saimon Msuva anaipatoa Tanzania bao la pili

VODEO. Tanzania Vs Botswana goli la msuva

Image

IPI INA VIEWER WENGI ZAIDI JIONEE HAPA seduce me vs zilipendwa

Image