SIR ALEX FURGASON AFANYIWA OPARESHENI YA KWA KICHWA.


Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana Mei 05, 2018 amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye kichwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Manchester United, imeelezwa kuwa upasuaji huo unahusisha ubongo na umeenda salama.

Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kuhusu tatizo linalomsumbua Mzee Ferguson hadi kufanyiwa upasuaji huo.

Kufuatia hali hiyo, Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye pia ni kocha wa klabu ya Doncaster jana alishindwa kuhudhuria mechi kati ya kalbu yake dhidi ya Wigan.

Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wametoa pole kwa mzee Ferguson kufuatia taarifa akiwemo Robin Van Persie, Pepe Reina, Diego Forlan, Bacary Sagna na wengineo.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya