Mzee Akili Mali: WACHEZAJI WENGI AMBAO HAWAJAJUMUIKA KWENDA ALGERIA WANAIDAI YANGA.
Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amefunguka kuhusiana na wachezaji wa Yanga waliokosekana katika msafara wa kuelekea Algeria jana kwa kusema kuwa wanadai.
Kikosi cha Yanga kimeondoka jana nchini kupitia Dubai kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.
Akilimali ameeleza kuwa wachezaji waliobaki hawajabi hivihivi na badala yake ameelez kuwa wanaidai klabu ndiyo maana hawajajumuika na timu.
Mjumbe huyo amesema kamwe hawezi kuwa mnafiki na akieleza kuwa msema ukweli siku zote ni mpenzi wa Mungu.
Wachezaji baadhi waliosalia nchini wakati Yanga ikikwea pipa jana ukiachana na wale majeruhi ni Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa na Kelvin Yondani.
Mbali na kutoa sababu hiyo, Akilimali ameitakia kheri Yanga kuelekea mchezo huo wa kwanza katika hatua ya makundi utakaopigwa Mei 6 2018, Jumapili ya wiki hii.
Comments
Post a Comment