MZEE MAJUTO KUPELEKWA INDIA LEO


Msanii wa filamu bongo Mzee Majuto leo Mei 1, 2018 anatarajiwa kusafiri na kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia matatizo aliyopata siku kadhaa zilizopita.

Steve Nyerere ambaye amehusika kwa namna moja au nyingine katika kusaidia kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee Majuto kwenda nchini India kwa matibabu zaidi amefunguka na kusema kuwa leo Mzee huyo atakwenda kwa matibabu zaidi nchini India na kuwataja watu ambao wamehusika katika kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe.

"Niseme ahsante sana Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Mwakyembe, Ummy Mwalimu na wadau pamoja na wasanii mbalimbali kwa kujitoa kwenu, Mzee wetu King Majuto Mungu akipenda leo atakuwa njiani kwenda India kwa matibabu zaidi"

Steve Nyerere hakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kuwataka wasanii wajifunze kupitia kwa Mzee Majuto kuwa kuna ulazima mkubwa wao kuwa na bima ya afya na kusema ni mkombozi kwao, anadai haiwezekani miaka nenda rudi wakawa ni watu wa kuombaomba kila wakati pindi wanapopata matatizo ili hali wanapata pesa za kutosha.

"Tuna kuombea kwa namna moja ama nyingine ,Baba naamini kwa maombi ya Watanzania utarudi katika kazi za ujenzi wa Taifa lako,Kuinua sanaa yetu,Kupeperusha bendera ya mkoa wako ,Baba kuumwa kwako kuna mafunzo mengi kwa wasanii na Watanzania kwa ujumla wake, Wasanii wenzangu bima ya afya ni kitu muhimu kwako na kwa familia yako, Bima ya Afya ni mwokozi kwetu. Sidhani kama miaka nenda rudi tutakuwa watu wa kuomba msaada ,tujiulize tunafanya mapart, tunakunywa na kusaza ,tunajinadi kwenye mitandao nguo zetu kuanzia milioni 3 mpaka 4 tukiulizwa umejipangaje kwa kesho amna kitu, ni muda wa kuamka sasa ,naamini majukumu hayakimbiliki bali tunayakabili" alisisitiza Steve Nyererere.

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya