KOCHA SIMBA.Tupo fit na tutawachapa Ndanda Leo.
Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre, amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Ndanda FC leo kwenye uwanja wa taifa huku lengo ni kuchukua alama tatu kuelekea ubingwa.
Akizungumza wakati wa mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo yaliyofanyika jana jioni, Lechantre ameweka wazi kuwa pointi tatu za leo ni muhimu sana katika kuiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa msimu huu.
''Tumemaliza maandalizi ya mchezo wetu wa kesho vizuri, lengo letu ni kushinda ili tupunguze alama zinazohitajika ili kuchukua ubingwa, kwahiyo tutajitahidi kuhakikisha tunashinda,'' amesema.
Simba na Ndanda FC zinakutana leo kwenye mchezo wa raundi ya 27 ligi kuu soka Tanzania Bara huku Simba ikiwa kileleni mwa msimamo wakati Ndanda FC ikiwa katika nafasi ya 15.
Simba SC ina pointi zake 62 baada ya mechi 26, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 49 za mechi 26 huku nafasi ya tata ikiwa na mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 48 kwenye mechi 24.
Comments
Post a Comment