HAWA HAPA WACHEZAJI 10 WA YANGA WALIOMALIZA MIKATABA YAO
Yanga ina idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu. Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria wa soka la Tanzanua, Mwinyi Zahera ndiye anayesubiriwa kuamua hatma ya wachezaji hao. Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika ni pamoja na Kelvini Yondani, Hassan Kessy, Juma Abdul, Andrew Vincent Chikupe na Obrey Chirwa. Wengine ni Nadir Haroub, Benno Kakolanya, Emmanuel Martin, Said Juma na Geofrey Mwashiuya