YANGA KUFUATA NYAYO ZA SIMBA.

Mambo yanabadilika kwa kasi kubwa na huenda itakuwa ni vigumu sana kuyazuia mabadiliko hasa katika klabu kongwe kama Yanga na Simba.

Simba wameanza na watani wao, Yanga nao wanaonekana wako njiani.

Kwani Kamati ya Mabadiliko ya Mfumo wa Uendeshaji wa Klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake, Wakili, Alex Mgongolwa kukutana kwa ajili ya kufikia muafaka.

Unaweza kusema ni neema inakaribia Yanga kwani mara baada ya kamati hiyo kukutana itapeleka ripoti kwenye Kamati ya Utendaji ya timu hiyo itakayotoa majibu kipi kifanyike.

Yanga wanataka kuleta mabadiliko hayo, ikiwa ni siku chache Simba kubadili mfumo wa uendeshaji wa timu hiyo kwa kumuuzia hisa mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji ‘Mo’.

Taarifa zinaeleza kamati hiyo ilikutana juzi Jumatatu usiku na kujadili mfumo wa mabadiliko hayo ya Klabu ya Yanga.

“Kamati yetu mpya tuliyoiteua ya Mabadiliko ya Uendeshaji wa klabu ilikutana juzi Jumatatu usiku na kikubwa ilikuwa makubaliano ya jinsi ya kuendesha klabu yetu ambayo inaturuhusu kikatiba.

“Na mifumo iliyopangwa kujadiliwa ni mfumo upi sahihi kati ya kampuni au kuuza hisa kwa muwekezaji kama ilivyokuwa kwa watani wetu wa jadi Simba.”

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia suala hilo, alisema: “Ni kweli kabisa kamati hiyo ilikutana lakini nisingependa kuweka wazi kila kitu hivi sasa.”


Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ya mfumo mpya wa mabadiliko ni Said Mecky Sadick, Profesa Mgongo Fimbo, Felix Mrema, George Fumbuka na Mohammed Nyengi

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya