DANTE AJITOA YANGA DK 180


By KHATIMU NAHEKA
BEKI wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ yuko jijini Dar es Salaam akiendelea na matibabu, lakini ametoa picha ya lini atarudi uwanjani kuendelea na majukumu yake, huku akikosa mechi mbili ukiondoa ya kesho ya kimataifa nchini Shelisheli.
Dante aliliambia Mwanaspoti bado anaendelea na tiba katika moja ya hospitali inayosimamiwa na raia wa China akiuguza majeraha yake ya nyama za paja.
Alisema kutokana na matibabu anayoendelea nayo atazikosa mechi mbili zijazo, dhidi ya Majimaji utakaopigwa mjini Songea ukiwa ni mchezo wa 16 Bora wa Kombe la FA na ule wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda mjini Mtwara.
Beki huyo mbishi alisema kutokana kupungua kwa maumivu kadri muda unavyosogea, huenda akarudi kazini katika mchezo wa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
“Kwa sasa naendelea vizuri kidogo japo bado nipo kwenye matibabu. Naona yananisaidia, hata hivyo, niliongea na daktari wangu na ameniambia sitaweza kucheza mechi mbili
zijazo,” alisema Dante.
“Kama mambo yataendelea vizuri kama yanavyoendelea sasa, ninaweza kurudi uwanjani katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar. Nadhani mpaka muda huo ukifika nitakuwa nimeshapona kabisa lakini hizi mechi mbili ndizo nina uhakika sitaweza kucheza

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya