MCHEZAJI HUYU WA YANGA AUGUA GHAFLA, SASA NI HATI HATI KUIVAA ST LOUIS HAPO KESHO.
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi yuko kwenye hatihati ya kutocheza mchezo wa kesho jioni dhidi ya St. Louis kutokana na kuugua ghafla asubuhi ya leo.
Mahadhi mfungaji wa bao pekee la Yanga katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam alishindwa hakuhudhuria mazoezi ya asubuhi na wenzake baada ya kusumbuliwa na tatizo la mafindofindo.
Baada ya kupatiwa matibabu asubuhi, Mahadhi hakuweza kufanya mazoezi na wenzake lengo likiwa ni kumpumzisha asipate madhara zaidi.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo alisema anaendelea vizuri na kuna uwezekano mkubwa akacheza kesho.
"Naendelea vizuri na kama Mungu akinijalia nikiamka salama, nitakuwa fiti kucheza mechi," alisema Mahadhi
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment