KIUNGO WA APR AIPA YANGA USHINDI
Shelisheli. Kiungo wa zamani wa Azam na nahodha wa APR, Baptiste Mugiraneza ameiombea dua zuri Yanga ili kufuzu hatua inayofuata.
Mugiraneza wamekutana na Yanga hapa Shelisheli kwa ajili ya mechi zao za marudiano kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho dhidi ya timu za hapa.
APR itafungua dimba kwa kucheza na Anse Reunion leo Jumanne kwenye Kombe la Shirikisho na siku inayofuata Yanga watacheza na St. Louis.
Hata hivyo pamoja na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi ya kwanza, Mugiraneza anaamini watasonga mbele kwenda hatua inayofuata.
"Yanga wako kwenye wakati mgumu kuliko sisi, lakini naamini watafanya vizuri kwenye mechi yao ya marudiano," alisema Mugiraneza.
Comments
Post a Comment