Posts

Showing posts from 2018

NEC yafanya uteuzi, CCM yaramba dume

Image
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteua madiwani nane wa Viti maalum wa CCM na CHADEMA kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika halmashauri nane za Tanzania bara, ambapo CCM yenyewe imefanikiwa kupata nafasi tano huku tatu zikienda CHADEMA. Hayo yamewekwa wazi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Julai 21, 2018 na kusema uteuzi huo umefanyika baada kukaa kikao cha tume hiyo cha Julai 19, 2018. Walioteuliwa ni Ajila Kalinga (CCM-Songea), Mary Kazindogo Mbilinyi (CCM Makete), Zainab Abdu Mabrouk (CCM-Kongwa), Restuta Aloyce Gardian (CCM-Muleba), Siglinda Silvester Ngwega (CCM-Morogoro). Wengine ni Zena Said Luzwilo (CCM-mji Kahama), Neema Michael Massawe (Chadema Monduli) na Teodola Muyula Kalungwana (Chadema-Iringa). "Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa aliitarifu tume ya uchaguzi kuwepo kwa nafasi hizo wazi

Yanga Yaleta Kiungo Kutoka Afrika Kusini

Image
   AKILI za viongozi wa Yanga zinaonekana hazipo tena kwenye Kombe la Shirikisho inayoendelea, kwani jana wachezaji waligoma lakini kuna kiungo kutoka Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Kingsley ametua kusajiliwa. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo irejee nchini ikitokea Kenya ilipokwenda kucheza na Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Yanga walifungwa mabao 4-0. Jana wachezaji waligoma kufanya mazoezi wakishinikiza wapewe chao lakini viongozi wanaonekana kuangalia zaidi msimu ujao. Yanga tayari imesajili wachezaji sita hadi hivi sasa ambao ni Mohamed Issa ‘Banka’, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Jaffary Mohamed, Heritier Makambo na Fei Toto . Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongoman, Mwinyi Zahera alisema kiungo huyo alitua hivi karibuni kwa siri nchini akitokea Sauzi alipokuwa akicheza soka kabla ya kukabidhiwa na kuanza majaribio. “Bado viongozi wanaendelea na usajili wao na kama unafahamu tayari nimewashauri viongozi wasajili wachezaji wengin

UMEIPATA HII KUHUSU GIGY MONEY.

Image
Video vixen Gigy na muimbaji Gigy Money amesema kwa sasa yupo pamoja na baba mtoto wake Mo Jay ikiwa ni miezi kadhaa toka wagombane na kurushiana maneno ya kashfa kupitia mitandao ya kijamii. Gigy amesema kwa sasa yupo tayari hata kumzalia watoto kwa kuwa amegundua mtangazaji huyo wa Choice FM ni mwanaume makini

KWELIIIIII!!!!!! NAMNA UNAVYOWEZA KUACHANA NA MCHEPUKO NA KUBAKI NJIABKUU.

Image
Habari za muda huu rafiki yangu, bila shaka u mzima na unaendelea na utaraitibu wako wa kila siku wa kutafuta griss ili kulaini vile vyuma vilivyokaza. Na siku ya leo naomba tujifunze kwa pamoja kuhusu ni kwa namna gani tunaweza kuachana na michepuko, kwani nimekuwa nikipokea jumbe nyingi sana za wasomaji wangu,  wengi wakiniuliza afisa mipango nifanye nini ili niweze kuachana na mchepuka na kubaki njia kuu? Nami bila hiana naomba nitirike hapa siku ya leo ili niwaponye wengi kwani swali la aina hii limekuwa likiwatesa wengi,  kwa sababu wengi wa wanaume au wanawake ambao wanachepuka imekuwa ni suala gumu sana kuweza kuondoka katika mchepuko na kubaki njia kuu. Mtego ambao umekuwa unatumiwa na michepuko kuwanasa wapenzi wa watu wengine, umekuwa upo vizuri kwa sababu pindi watu wanasapo imekuwa ni ngumu sana kunasuka. Kama na wewe ni miongoni mwa watu hao ambao wamekuwa wakichepuka na wameshindwa kunasuka unachotakiwa kufanya ni; 1. Unapokuwa upo pamoja na mchepuko au wahenga wa hivi

YANGA KUJITOA KAGAME CUP.

Image
Tetesi zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga imeiandikia barua Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam. Sababu za msingi ziliifanya Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi. Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda. Eatv.tv imemtafuta Katibu wa klabu hiyo Boniphace Mkwassa ambaye amethibitisha kuwa Kamati ya Utendaji wa klabu, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao. Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo w

HAWA HAPA WACHEZAJI 10 WA YANGA WALIOMALIZA MIKATABA YAO

Image
Yanga ina idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu. Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria wa soka la Tanzanua, Mwinyi Zahera ndiye anayesubiriwa kuamua hatma ya wachezaji hao. Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika ni pamoja na Kelvini Yondani, Hassan Kessy, Juma Abdul, Andrew Vincent Chikupe na Obrey Chirwa. Wengine ni Nadir Haroub, Benno Kakolanya, Emmanuel Martin, Said Juma na Geofrey Mwashiuya

Baada ya kufungwa Jana Yanga yashika nafasi ya mwisho.

Image
Mabingwa wa soka nchini Yanga, wamepoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ugenini dhidi ya U.S.M Alger kwa mabao 4-0 na kushika mkia katika kundi la la D. Mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Algiers, Yanga iliruhusu mabao mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongezwa mengine mawili kipindi cha pili na kufanya waondoke bila alama huku wakiwa na deni kubwa la mabao ya kufungwa. Katika Kundi D, Yanga inashika nafasi ya nne ambayo ni ya mwisho baada ya mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa usiku huo huo kati ya wenyeji Rayon Sport ambao walitoka sare ya bao 1-1 na  Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. Kwenye ligi kuu Tanzania Bara, Yanga inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC ikiwa na alama 48 kwenye mechi 24 ilizocheza hadi sasa. Azam ina alama 49 kwenye mechi 27 na Simba ina pointi 65 baada ya mechi 27. Kundi D sasa linaongozwa na U.S.M Alger yenye alama 3 ikifuatiwa na Gor Mahia yenye alama 1 sawa na R

SIR ALEX FURGASON AFANYIWA OPARESHENI YA KWA KICHWA.

Image
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana Mei 05, 2018 amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye kichwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Manchester United, imeelezwa kuwa upasuaji huo unahusisha ubongo na umeenda salama. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kuhusu tatizo linalomsumbua Mzee Ferguson hadi kufanyiwa upasuaji huo. Kufuatia hali hiyo, Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye pia ni kocha wa klabu ya Doncaster jana alishindwa kuhudhuria mechi kati ya kalbu yake dhidi ya Wigan. Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wametoa pole kwa mzee Ferguson kufuatia taarifa akiwemo Robin Van Persie, Pepe Reina, Diego Forlan, Bacary Sagna na wengineo.

KOCHA SIMBA.Tupo fit na tutawachapa Ndanda Leo.

Image
Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre, amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Ndanda FC leo kwenye uwanja wa taifa huku lengo ni kuchukua alama tatu kuelekea ubingwa. Akizungumza wakati wa mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo yaliyofanyika jana jioni, Lechantre ameweka wazi kuwa pointi tatu za leo ni muhimu sana katika kuiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa msimu huu. ''Tumemaliza maandalizi ya mchezo wetu wa kesho vizuri, lengo letu ni kushinda ili tupunguze alama zinazohitajika ili kuchukua ubingwa, kwahiyo tutajitahidi kuhakikisha tunashinda,'' amesema. Simba na Ndanda FC zinakutana leo kwenye mchezo wa raundi ya 27 ligi kuu soka Tanzania Bara huku Simba ikiwa kileleni mwa msimamo wakati Ndanda FC ikiwa katika nafasi ya 15. Simba SC ina pointi zake 62 baada ya mechi 26, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 49 za mechi 26 huku nafasi ya tata ikiwa na mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 48 kwenye mechi 24.

HATIMAYE YANGA WAFUNGUKA UKWELI KUHUSU UCHUMI NA MTIKISIKO WA KIUCHUMI NDANI YA CLUB HIYO.

Image
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Msemaji wake, Dismas Teni, umeeleza kwa msisitizo kuwa ni kweli unapitia wakati mgumu hivi baada ya kuyumba kuyumba kiuchumi. Ten ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya USM katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger huko Algeria. Ofisa huyo wa Habari amesema Yanga hivi sasa ina tatizo la kuyumba kiuchumi, huku akieleza kuwa ni timu nyingi huwa zinapitia changamoto kama hizo na akiamini siku moja suala hilo litapita. Yanga imekuwa haina matokeo mazuri msimu katika ligi na mashindano ya kimataifa ukilingana na msimu mmoja nyuma, sababu za kuyumba kwa uchumi zinaelezwa kuchangia pia kikosi kutokuwa imara. Katika mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho, Yanga itakuwa inawakosa wachezaji wake kadhaa walio mhimili wa kikosi cha kwanza.

MKWASA AWAKINGIA KIFUA WACHEZAJI AMBAO HAWAJASAFIRI NA TIMU KWENDA ALGERIA.

Image
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa ufafanuzi juu ya wachezaji wake muhimu, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshimbi kutojumuika na kikosi kilichosafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya USM Alger. Mkwasa amesema kuwa wachezaji wote waliyoshindwa kujiunga na Yanga kwenye safari hiyo walikuwa na sababu zao muhimu nawala siyo mambo mengine kama yanavyoelezwa. Kunasababu mbalimbali kwa wachezaji kupelekea wao kutokusafari, rabda nikianza na Kelvin Yondani yeye alipata majeraha wakati wa mechi na Simba na alipoomba atoke tukashindwa mkutoa kwasababu mechi ilikuwa tayari ilishamalizika. Mchezaji wa pili ni Obrey Chirwa alikuwa na Malaria na baada ya mechi ikaongezeka kwahiyo ikashindikana kusafiri. Mchezaji wa tatu ni Ajib, yeye yupo fiti ila anamatatizo ya kifamilia Mkewake anatarajia kujifungua muda wowote na hivyo kunahitaji uwangalizi wa hali ya juu kwahiyo anahitajika awe karibu ndiyo m

Yanga Yafunguka Sababu ya Ajibu, Shishimbi na Chirwa Kutokwenda Algeria.

Image
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa ufafanuzi juu ya wachezaji wake muhimu, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshimbi kutojumuika na kikosi kilichosafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya USM Alger. Mkwasa amesema kuwa wachezaji wote waliyoshindwa kujiunga na Yanga kwenye safari hiyo walikuwa na sababu zao muhimu nawala siyo mambo mengine kama yanavyoelezwa. Kunasababu mbalimbali kwa wachezaji kupelekea wao kutokusafari, rabda nikianza na Kelvin Yondani yeye alipata majeraha wakati wa mechi na Simba na alipoomba atoke tukashindwa mkutoa kwasababu mechi ilikuwa tayari ilishamalizika. Mchezaji wa pili ni Obrey Chirwa alikuwa na Maleria na baada ya mechi ikaongezeka kwahiyo ikashindikana kusafiri. Mchezaji wa tatu ni Ajib, yeye yupo fiti ila anamatatizo ya kifamilia Mkewake anatarajia kujifungua muda wowote na hivyo kunahitaji uwangalizi wa hali ya juu kwahiyo anahitajika awe karibu nd

KELVIN YONDANI HATIHATI KUTIMIKIA SIMBA.Mpaka muda wa kuondoka KWENDA Algeria Simu yake ilikuwa haipatikani.

Image
Wakati Yanga wakihaha kum­bakisha beki mkongwe wa kati, Kelvin Yondani watani wao wa jadi Simba nao wame­ingia rada za kuhakikisha wanainasa saini ya nyota huyo. Beki huyo, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayomhitaji kwa ajili ya kuichezea katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya mkataba wake ku­malizika mwezi huu Mei. Yondani ni kati ya mabeki bora katika msimu huu wa ligi kutokana na kucheza vema katika nafasi hiyo ya kati am­bapo hivi sasa anawindwa na timu kadhaa ikiwemo Azam FC. Kwa mujibu wa taarifa am­bazo imezipata uon­gozi wa Yanga, wana taarifa za beki huyo kuwindwa na Simba kwa ajili ya kumsajili na kinachowachanganya zaidi ni kutokuwepo kambini pamoja na wenzake. Mtoa taarifa huyo alisema, beki huyo tayari amewaam­bia viongozi wa timu juu ya kuwindwa na Simba baada ya kupokea simu nyingi kutoka kwa mabosi wa Msimbazi kuonyesha nia ya kumsajili. “Sisi wenyewe Yanga ndiyo tunamuwekea mazingira ya kuondoka Yondani kwenda Simb

Mzee Akili Mali: WACHEZAJI WENGI AMBAO HAWAJAJUMUIKA KWENDA ALGERIA WANAIDAI YANGA.

Image
Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amefunguka kuhusiana na wachezaji wa Yanga waliokosekana katika msafara wa kuelekea Algeria jana kwa kusema kuwa wanadai. Kikosi cha Yanga kimeondoka jana nchini kupitia Dubai kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger. Akilimali ameeleza kuwa wachezaji waliobaki hawajabi hivihivi na badala yake ameelez kuwa wanaidai klabu ndiyo maana hawajajumuika na timu. Mjumbe huyo amesema kamwe hawezi kuwa mnafiki na akieleza kuwa msema ukweli siku zote ni mpenzi wa Mungu. Wachezaji baadhi waliosalia nchini wakati Yanga ikikwea pipa jana ukiachana na wale majeruhi ni Ibrahim Ajibu, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa na Kelvin Yondani. Mbali na kutoa sababu hiyo, Akilimali ameitakia kheri Yanga kuelekea mchezo huo wa kwanza katika hatua ya makundi utakaopigwa Mei 6 2018, Jumapili ya wiki hii. Shiriki sasa na ujinyakulie mtonyo.BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI USISAHAU UNAWEZA JISHINDIA MPAKA 100000 CHAP CHAP

Lwandamila atua rasmi Zesco.

Image
Kocha wa zamani wa Yanga, George Lwandamina, rasmi ametambulishwa na uongozi wa Zesco United ya Zambia kuwa Mwalimu Mkuu wa timu hiyo. Lwandamina alirejea nchini kwao kimyakimya akiiacha Yanga kutokana na madai ya fedha za mishahara ambazo hajalipwa. Zesco wameamua kumrejesha tena Lwandamina wakiwa na imani kuwa atakisaidia kikosi hicho kufanya vizuri katika mashindano ya ligi na kimataifa. Lwandamina ametambulishwa jana wakati Yanga ikiwa tayari imeshaanza kazi na Mkongomani mpya, Mwinyi Zahera aliyekuja nchini hivi karibuni kuchukua mikoba yake. JISHINDIE KUANZIA 10,000/= HADI 100,000 BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI UNAWEZAJE KUSHINDA SASA

HAJI MANARA ATUMIWA SALAM NA WEMA SEPETU.

Image
Msanii Wema Sepetu, ametuma salamu kwa mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara, na kutamba kwa kusema, klabu ya Yanga ndio timu kubwa na yenye mafanikio hapa nchini na kitendo cha kufungwa na Simba katika mchezo wa April 29 ni sehemu ya mchezo tu. Akiongea na waandishi wa habari Jana Mei 02 wakati wa kutambulishwa kama balozi wa Startimes kueleka kombe la dunia, Wema amesema yeye ni mpenzi mkubwa wa timu Yanga na hata katika kuchukua ubingwa timu hiyo imefanikiwa zaidi kuliko wapizani wao simba. “Mpelekeeni salamu Haji Manara, anajua kabisa kwamba Yanga tumechukua ligi (kuu bara) mara nyingi sana, kwa hiyo wao (Simba) kutufunga juzi ni changamoto, katika ubingwa huwa tunawachapa kilasiku”, amesema Wema Haji Manara na msanii Wema Sepetu wamekua na tambo za maneno kuhusu timu za Simba Yanga hususani katika mitandao ya kijamii. Akiongelea kuhusu nchi wakilishi wa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia Wema amesema, bado kuna changamoto kubwa kwa nchi hizo k

MZEE MAJUTO KUPELEKWA INDIA LEO

Image
Msanii wa filamu bongo Mzee Majuto leo Mei 1, 2018 anatarajiwa kusafiri na kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia matatizo aliyopata siku kadhaa zilizopita. Steve Nyerere ambaye amehusika kwa namna moja au nyingine katika kusaidia kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee Majuto kwenda nchini India kwa matibabu zaidi amefunguka na kusema kuwa leo Mzee huyo atakwenda kwa matibabu zaidi nchini India na kuwataja watu ambao wamehusika katika kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe. "Niseme ahsante sana Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Mwakyembe, Ummy Mwalimu na wadau pamoja na wasanii mbalimbali kwa kujitoa kwenu, Mzee wetu King Majuto Mungu akipenda leo atakuwa njiani kwenda India kwa matibabu zaidi" Steve Nyerere hakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kuwataka wasanii wajifunze kupitia kwa Mzee Majuto kuwa kuna ulazima mkubwa wao kuwa na bima ya afya na kusema ni mkombozi kwao, anad

NGOMA AJUTIA MAAMUZI YAKE NDANI YA YANGA.

Image
Ishu ya Donald Ngoma kupitia kwa Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, ameandika machache kuhusiana na mchezaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Donald Ngoma, ambaye hajaonekana Uwanjani kwa muda mrefu. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Teni ameandika ujumbe akieleza kuwa maisha ni changamoto hivyo kuna wakati lazima uzipitie ili uweze kushinda. "Ndiyo maana yakaitwa maisha, kuna wakati ni lazima upitie changamoto ili kuyashindao Bofya hapa kuona goli la Simba 1 vs Yanga 0.

TUJUKUMBUSHE KIDOGO MATOKEO TOKA 1965 MPAKA 2017,Yanga aendelea kuongoza kwa matokeo na points.

Image
REKODI YA SIMBA NA YANGA LIGI KUU PEKEE P W D L Pts  Yanga SC 98 36 33 26 113 Simba SC 98 26 33 36 83 MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA ZA WATANI WA JADI; JUNI 7, 1965 Yanga v Sunderland (Simba) 1-0 MFUNGAJI: Mawazo Shomvi dk. 15). JUNI 3, 1966 Yanga v Sunderland (Simba) 3-2 WAFUNGAJI: Yanga: Abdulrahman Lukongo dk. 54, Andrew Tematema dk 67, Emmanuel Makaidi dk. 83. Sunderland: Mustafa Choteka dk 24, Haji Lesso dk. 86. NOVEMBA 26, 1966 Sunderland v Yanga 1-0 MFUNGAJI: Mustafa Choteka dk. 44. MACHI 30, 1968 Yanga v Sunderland 1-0 MFUNGAJI: Kitwana Manara dk. 28. JUNI 1, 1968 Yanga v Sunderland 5-0 WAFUNGAJI: Maulid Dilunga dk. 18 (penalti), Dilunga dk. 43, Salehe Zimbwe dk. 54, Zimbwe dk. 89, Kitwana Manara dk. 86. MACHI 3, 1969 Yanga v Sunderland (Yanga ilipewa pointi za chee na ushindi wa mabao 2-0, baada ya Sunderland kugoma kuingia uwanjani). JUNI 4, 1972 Yanga v Sunderland 1-1 WAFUNGAJI: Yanga: Kitwana Manara dk. 19, Sunderland: Willy Mwaijibe dk.