Posts

UMEIPATA HII KUHUSU GIGY MONEY.

Image
Video vixen Gigy na muimbaji Gigy Money amesema kwa sasa yupo pamoja na baba mtoto wake Mo Jay ikiwa ni miezi kadhaa toka wagombane na kurushiana maneno ya kashfa kupitia mitandao ya kijamii. Gigy amesema kwa sasa yupo tayari hata kumzalia watoto kwa kuwa amegundua mtangazaji huyo wa Choice FM ni mwanaume makini

KWELIIIIII!!!!!! NAMNA UNAVYOWEZA KUACHANA NA MCHEPUKO NA KUBAKI NJIABKUU.

Image
Habari za muda huu rafiki yangu, bila shaka u mzima na unaendelea na utaraitibu wako wa kila siku wa kutafuta griss ili kulaini vile vyuma vilivyokaza. Na siku ya leo naomba tujifunze kwa pamoja kuhusu ni kwa namna gani tunaweza kuachana na michepuko, kwani nimekuwa nikipokea jumbe nyingi sana za wasomaji wangu,  wengi wakiniuliza afisa mipango nifanye nini ili niweze kuachana na mchepuka na kubaki njia kuu? Nami bila hiana naomba nitirike hapa siku ya leo ili niwaponye wengi kwani swali la aina hii limekuwa likiwatesa wengi,  kwa sababu wengi wa wanaume au wanawake ambao wanachepuka imekuwa ni suala gumu sana kuweza kuondoka katika mchepuko na kubaki njia kuu. Mtego ambao umekuwa unatumiwa na michepuko kuwanasa wapenzi wa watu wengine, umekuwa upo vizuri kwa sababu pindi watu wanasapo imekuwa ni ngumu sana kunasuka. Kama na wewe ni miongoni mwa watu hao ambao wamekuwa wakichepuka na wameshindwa kunasuka unachotakiwa kufanya ni; 1. Unapokuwa upo pamoja na mchepuko au wahenga...

YANGA KUJITOA KAGAME CUP.

Image
Tetesi zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga imeiandikia barua Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam. Sababu za msingi ziliifanya Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi. Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda. Eatv.tv imemtafuta Katibu wa klabu hiyo Boniphace Mkwassa ambaye amethibitisha kuwa Kamati ya Utendaji wa klabu, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao. Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo w...

HAWA HAPA WACHEZAJI 10 WA YANGA WALIOMALIZA MIKATABA YAO

Image
Yanga ina idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu. Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria wa soka la Tanzanua, Mwinyi Zahera ndiye anayesubiriwa kuamua hatma ya wachezaji hao. Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika ni pamoja na Kelvini Yondani, Hassan Kessy, Juma Abdul, Andrew Vincent Chikupe na Obrey Chirwa. Wengine ni Nadir Haroub, Benno Kakolanya, Emmanuel Martin, Said Juma na Geofrey Mwashiuya

Baada ya kufungwa Jana Yanga yashika nafasi ya mwisho.

Image
Mabingwa wa soka nchini Yanga, wamepoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ugenini dhidi ya U.S.M Alger kwa mabao 4-0 na kushika mkia katika kundi la la D. Mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Algiers, Yanga iliruhusu mabao mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongezwa mengine mawili kipindi cha pili na kufanya waondoke bila alama huku wakiwa na deni kubwa la mabao ya kufungwa. Katika Kundi D, Yanga inashika nafasi ya nne ambayo ni ya mwisho baada ya mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa usiku huo huo kati ya wenyeji Rayon Sport ambao walitoka sare ya bao 1-1 na  Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. Kwenye ligi kuu Tanzania Bara, Yanga inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC ikiwa na alama 48 kwenye mechi 24 ilizocheza hadi sasa. Azam ina alama 49 kwenye mechi 27 na Simba ina pointi 65 baada ya mechi 27. Kundi D sasa linaongozwa na U.S.M Alger yenye alama 3 ikifuatiwa na Gor Mahia yenye alama 1 sawa ...

SIR ALEX FURGASON AFANYIWA OPARESHENI YA KWA KICHWA.

Image
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana Mei 05, 2018 amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye kichwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Manchester United, imeelezwa kuwa upasuaji huo unahusisha ubongo na umeenda salama. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kuhusu tatizo linalomsumbua Mzee Ferguson hadi kufanyiwa upasuaji huo. Kufuatia hali hiyo, Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye pia ni kocha wa klabu ya Doncaster jana alishindwa kuhudhuria mechi kati ya kalbu yake dhidi ya Wigan. Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wametoa pole kwa mzee Ferguson kufuatia taarifa akiwemo Robin Van Persie, Pepe Reina, Diego Forlan, Bacary Sagna na wengineo.

KOCHA SIMBA.Tupo fit na tutawachapa Ndanda Leo.

Image
Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre, amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Ndanda FC leo kwenye uwanja wa taifa huku lengo ni kuchukua alama tatu kuelekea ubingwa. Akizungumza wakati wa mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo yaliyofanyika jana jioni, Lechantre ameweka wazi kuwa pointi tatu za leo ni muhimu sana katika kuiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa msimu huu. ''Tumemaliza maandalizi ya mchezo wetu wa kesho vizuri, lengo letu ni kushinda ili tupunguze alama zinazohitajika ili kuchukua ubingwa, kwahiyo tutajitahidi kuhakikisha tunashinda,'' amesema. Simba na Ndanda FC zinakutana leo kwenye mchezo wa raundi ya 27 ligi kuu soka Tanzania Bara huku Simba ikiwa kileleni mwa msimamo wakati Ndanda FC ikiwa katika nafasi ya 15. Simba SC ina pointi zake 62 baada ya mechi 26, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 49 za mechi 26 huku nafasi ya tata ikiwa na mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 48 kwenye mechi 24.