MGOMBEA YANGA ATOA AHADI NZITO NZITO



Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika Klabu ya Yanga Magege Chota, ameahidi kulipa fedha zote za mishahara endapo atachaguliwa.

Mgombea huyo amesema kuwa Yanga hivi sasa inapitia wakati mgumu kiasi cha kwamba wachezaji wamekuwa wakicheza bila kutimiziwa stahiki zao.

Chota ameeleza suala hilo litakuwa ni la kwanza kuanza kulitekeleza ili kuondoa mkanganyiko uliopo hivi sasa ndani ya kikosi ambapo kuna baadhi ya wachezaji wamekuwa wakigoma.

"Unaua wachezaji wa Yanga wengi hawajalipwa fedha za mishahara yao, nawaahidi wanachama wa Yanga kuwa nitafanya zoezi la kuwalipa wachezaji ili vita ya mapambano ishike kasi endapo wakinipa kura" alisema Chota

Mwanachama huyo ameanza kampeni zake rasmi baada ya hapo jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuthibitisha kuwa muda wa kampeni umeshaanza na utachukua siku tano

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya