Posts

YANGA KUJITOA KAGAME CUP.

Image
Tetesi zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga imeiandikia barua Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF), kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam. Sababu za msingi ziliifanya Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi. Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda. Eatv.tv imemtafuta Katibu wa klabu hiyo Boniphace Mkwassa ambaye amethibitisha kuwa Kamati ya Utendaji wa klabu, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao. Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo w...

HAWA HAPA WACHEZAJI 10 WA YANGA WALIOMALIZA MIKATABA YAO

Image
Yanga ina idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu. Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Kihistoria wa soka la Tanzanua, Mwinyi Zahera ndiye anayesubiriwa kuamua hatma ya wachezaji hao. Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika ni pamoja na Kelvini Yondani, Hassan Kessy, Juma Abdul, Andrew Vincent Chikupe na Obrey Chirwa. Wengine ni Nadir Haroub, Benno Kakolanya, Emmanuel Martin, Said Juma na Geofrey Mwashiuya

Baada ya kufungwa Jana Yanga yashika nafasi ya mwisho.

Image
Mabingwa wa soka nchini Yanga, wamepoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ugenini dhidi ya U.S.M Alger kwa mabao 4-0 na kushika mkia katika kundi la la D. Mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo jijini Algiers, Yanga iliruhusu mabao mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongezwa mengine mawili kipindi cha pili na kufanya waondoke bila alama huku wakiwa na deni kubwa la mabao ya kufungwa. Katika Kundi D, Yanga inashika nafasi ya nne ambayo ni ya mwisho baada ya mechi nyingine ya kundi hilo iliyopigwa usiku huo huo kati ya wenyeji Rayon Sport ambao walitoka sare ya bao 1-1 na  Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. Kwenye ligi kuu Tanzania Bara, Yanga inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC ikiwa na alama 48 kwenye mechi 24 ilizocheza hadi sasa. Azam ina alama 49 kwenye mechi 27 na Simba ina pointi 65 baada ya mechi 27. Kundi D sasa linaongozwa na U.S.M Alger yenye alama 3 ikifuatiwa na Gor Mahia yenye alama 1 sawa ...

SIR ALEX FURGASON AFANYIWA OPARESHENI YA KWA KICHWA.

Image
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson jana Mei 05, 2018 amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye kichwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Manchester United, imeelezwa kuwa upasuaji huo unahusisha ubongo na umeenda salama. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kuhusu tatizo linalomsumbua Mzee Ferguson hadi kufanyiwa upasuaji huo. Kufuatia hali hiyo, Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye pia ni kocha wa klabu ya Doncaster jana alishindwa kuhudhuria mechi kati ya kalbu yake dhidi ya Wigan. Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wametoa pole kwa mzee Ferguson kufuatia taarifa akiwemo Robin Van Persie, Pepe Reina, Diego Forlan, Bacary Sagna na wengineo.

KOCHA SIMBA.Tupo fit na tutawachapa Ndanda Leo.

Image
Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre, amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Ndanda FC leo kwenye uwanja wa taifa huku lengo ni kuchukua alama tatu kuelekea ubingwa. Akizungumza wakati wa mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo yaliyofanyika jana jioni, Lechantre ameweka wazi kuwa pointi tatu za leo ni muhimu sana katika kuiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa msimu huu. ''Tumemaliza maandalizi ya mchezo wetu wa kesho vizuri, lengo letu ni kushinda ili tupunguze alama zinazohitajika ili kuchukua ubingwa, kwahiyo tutajitahidi kuhakikisha tunashinda,'' amesema. Simba na Ndanda FC zinakutana leo kwenye mchezo wa raundi ya 27 ligi kuu soka Tanzania Bara huku Simba ikiwa kileleni mwa msimamo wakati Ndanda FC ikiwa katika nafasi ya 15. Simba SC ina pointi zake 62 baada ya mechi 26, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 49 za mechi 26 huku nafasi ya tata ikiwa na mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 48 kwenye mechi 24.

HATIMAYE YANGA WAFUNGUKA UKWELI KUHUSU UCHUMI NA MTIKISIKO WA KIUCHUMI NDANI YA CLUB HIYO.

Image
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Msemaji wake, Dismas Teni, umeeleza kwa msisitizo kuwa ni kweli unapitia wakati mgumu hivi baada ya kuyumba kuyumba kiuchumi. Ten ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya USM katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger huko Algeria. Ofisa huyo wa Habari amesema Yanga hivi sasa ina tatizo la kuyumba kiuchumi, huku akieleza kuwa ni timu nyingi huwa zinapitia changamoto kama hizo na akiamini siku moja suala hilo litapita. Yanga imekuwa haina matokeo mazuri msimu katika ligi na mashindano ya kimataifa ukilingana na msimu mmoja nyuma, sababu za kuyumba kwa uchumi zinaelezwa kuchangia pia kikosi kutokuwa imara. Katika mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho, Yanga itakuwa inawakosa wachezaji wake kadhaa walio mhimili wa kikosi cha kwanza.

MKWASA AWAKINGIA KIFUA WACHEZAJI AMBAO HAWAJASAFIRI NA TIMU KWENDA ALGERIA.

Image
Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa ufafanuzi juu ya wachezaji wake muhimu, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshimbi kutojumuika na kikosi kilichosafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya USM Alger. Mkwasa amesema kuwa wachezaji wote waliyoshindwa kujiunga na Yanga kwenye safari hiyo walikuwa na sababu zao muhimu nawala siyo mambo mengine kama yanavyoelezwa. Kunasababu mbalimbali kwa wachezaji kupelekea wao kutokusafari, rabda nikianza na Kelvin Yondani yeye alipata majeraha wakati wa mechi na Simba na alipoomba atoke tukashindwa mkutoa kwasababu mechi ilikuwa tayari ilishamalizika. Mchezaji wa pili ni Obrey Chirwa alikuwa na Malaria na baada ya mechi ikaongezeka kwahiyo ikashindikana kusafiri. Mchezaji wa tatu ni Ajib, yeye yupo fiti ila anamatatizo ya kifamilia Mkewake anatarajia kujifungua muda wowote na hivyo kunahitaji uwangalizi wa hali ya juu kwahiyo anahitajika awe karibu ndiyo m...