Posts

Mchezaji Said Hamis Juma ‘Ndemla’ amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.

Image
Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja. Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko. Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla. Wakati huohuo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi. Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017. Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ti...

Hivi Ndivyo Dkt Shika Anavyokula Bata la Uzeeni

Image
Dk Louis Shika ambaye katika siku za hivi karibuni amejipatia umaarufu mkubwa, juzikati amefunguka kuwa ‘bata’ la uzeeni analokula sasa hivi ni balaa kutokana na michongo ya fedha anayopata. Akipiga stori na Risasi Jumamosi juzi, Dk. Shika alisema kuwa, wakati akisubiria fedha zake za Urusi, sasa hivi amekuwa akipata madili ya fedha na kuyabadili maisha yake. Mmoja wa mameneja wa Dk. Shika ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, amethibitisha kwamba tangu aanze kumsimamia mzee huyo, amekuwa akipata michongo kibao kila siku. TUMSIKILIZE MENEJA “Daah kwa kweli ni michongo mingi sana ya hela. Yaani simu kila wakati inaita. Watu wanamhitaji kweli Dk. Shika, kwa siku napokea si chini ya simu hamsini mpaka sitini,” alisema meneja huyo. AZICHUJA SIMU Meneja huyo alisema, baada ya kuona simu hizo zimekuwa nyingi, wamelazimika kuwa wanazichuja kulingana na namna mtu anavyojieleza kwani wengi wao wamekuwa wakitoa michongo ya fedha ndogo. “Unakuta mwingine anakuambia eti anataka kupiga...

Dkt Shika Apata Shavu la Matangazo na Huu ndo Muonekano Wake Mpya

Image
Maisha ya Dk Louis Shika ambaye hivi karibuni aliingia kwenye headline baada ya kushindwa kutoa asilimia 25 ya mnada wa nyumba za Lugumi muda mchache baada ya kushinda mnada huo, yameanza kubadilika taratibu kutokana na kupata deal kadhaa za matangazo. DK Shika ambaye alikuwa katika muonekano ambao haufananii na utajiri anaoutangaza kuwa nao, weekend hii ameonekana akiwa amevaa suti kali. Wadau wa mambo wanadai kuwa mzee huyo mashuhuri mitandaoni amepata deal kubwa katika kampuni moja kubwa la michezo ya kubashiri. Huwenda akapata deal nyingi zaidi kutoka na umaarufu alionao kwa sasa

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHO VAANA NA PRISON LEO HIKI HAPA

Image
Yanga wanaokwenda Chamazi kuwava Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, leo, hawa hapa.. 1. Youthe Rostand 2. Juma Abdul 3. Gadiel Michael 4. Andrew Vincent 5. Nadir Haroub 6. Pato Ngonyani 7. Pius Buswita 8. Raphael Daud 9. Obrey Chirwa 10. Ibrahim AjibU 11. Emmanuel Martin AKIBA:  Beno Kakolanya Hassan Kessy Maka Edward Yusuph Mhilu Said Mussa  Geofrey Mwashiuya

Mbeya City Yalazimika Kufanya Mabadiliko ya Dharura

Image
Klabu ya soka ya Mbeya City imelazimika kubadili jezi yake iliyokuwa imepanga kuitumia kwenye mechi ya ugenini leo dhidi ya Singida United. Mbeya City imefikia uamzi huo baada ya kuwepo kwa mfanano kati ya jezi yake ya Singida United ambao ni wenyeji wao katika mchezo wa leo. Jezi hizo ni kama zinavyoonekana hapo chini ambapo kushoto ni jezi ya wenyeji Singida United na kulia ni jezi ya Mbeya City iliyokuwa imepangwa kutumika leo. Hata hivyo bado Mbeya City hawajasema ni jezi gani ambayo watatumia lakini msimu huu jezi zao za pili kwaajili ya mechi za ugenini ni zile zenye rangi ya damu ya mzee hivyo huenda ndio zitakazotumika leo. Singida United inayoshika nafasi ya 5 ikiwa na alama 17 inacheza leo na Mbeya City yenye alama 11 katika nafasi ya 10 kwenye mchezo wa raundi ya 11, uwanja wa Namfua mjini Singida

“Wapiga Penati Wanaangalia Chini Kama Kondoo, Enzi zangu Bwana…”-Mwakyembe Atoa Somo Upigaji Penati

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa somo kwa wanasoka wa Tanzania kuhusu namna ya upigaji wa penati baada ya kutoridhishwa na namna ya baadhi ya wachezaji wanaopiga matuta nchini. Waziri Mwakyembe amesema enzi zake alikuwa anawatungua magolikipa kwa mikwaju ya matuta tofauti na wapigaji wa siku hizi ambao huangalia chini mithili ya kondoo anaetaka kupigana. “Upigaji penati nchi hii nafikiri nahitaji kukaa na makocha, sisi zamani tulikuwa tunafundishwa. Pale alikuwa hakosi penati, lakini vijana wa sikuhizi pamoja na ufundi mkubwa walionao, wanapiga penati wameangalia chini. Inashangaza mtu anaangaliaje chini? Wanabahatisha.” “Mimi sipigi penati naangalia chini, najua toka niliposimama hadi kwenye mpira ni hatua sita, namwangalia golikipa movements zake, mguu wangu unaponyanyuka akianza kwenda kulia, mimi napiga kushoto, ndio upigaji wa penati. sasa mtu anaangalia chini utafikiri kondoo anakwenda kupigana.” “Mimi ni mchezaji wa soka wa muda m...

Tamasha la Fiesta Kimeeleweka Hadi Majogoo Wasanii Walioondolewa Warudishwa

Image
Ilitangazwa kwamba Tamasha kubwa la FIESTA 2017 Mkoa wa Dar es salaam litafanyika mpaka saa saba usiku ambapo taarifa hizo zikafanya kamati kuwaondoa Wasanii zaidi ya 15 kwenye orodha ya kutumbuiza sababu ya badiliko la muda wa kumaliza sherehe hii kubwa ya Taifa la Bongofleva. Wasanii wote walioondolewa wamerudishwa kwenye orodha na mipango yao ya kazi itaendelea kama kawa Tayari kupunguzwa huko kwa muda kulishafanya baadhi ya Wasanii waondolewe kwenye orodha ya Wanaotumbuiza kwenye tamasha hilo akiwemo Lulu Diva. USISAHAU KUANGALIA VIDEO YA ASLAY ALIVYO BURUNDISHA KWA USTADI WATU WA IRINGA TIGO FIESTA.