Mkojo wa Wema watikisa Mahakamani

KESI inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, jana ilichukua sura mpya baada ya mawakili wa pande mbili, ule wa utetezi na Jamhuri kuchuana kuhusu mkojo wa msanii huyo uliochukuliwa na kupimwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa upelelezi wa polisi kuhusiana na mwanadada huyo kudaiwa kutumia madawa ya kulevya. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri aliyefahamika kwa jina la Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akisoma ripoti ya uchunguzi alisema mahakamani hapo kuwa, mkojo wa Wema baada ya kupimwa ulikutwa na chembechembe za bangi. Hata hivyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema ripoti hiyo iliyosomwa na Mulima ina upungufu mwingi wa kisheria. Baada ya kutokea malumbano hayo Hakimu Mkazi Simba aliwaomba mawakili wa pande zote mbili kuridhia apate muda wa kuipitia taarifa hiyo ya Ofisi ya Mkemia Mkuu ili itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi. Awali, kesi hiyo iliahirishwa kusi...