JAMAL Malinzi (57), Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufikishwa mahakamani mchana huu jijini Dar es Salaam, kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. Taarifa kutoka ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) zinasema, Malinzi anafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako anatarajiwa kukabiliwa na mashitaka kadhaa ya ufujaji wa fedha za shirikisho, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Mbali na Malinzi mwingine anayefikishwa mahakamani pamoja naye, ni katibu mkuu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa. “Ndio. Rais wa TFF na katibu mkuu wake, wote wawili tunawashikilia na watafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma zinazowakabili,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa Takukuru ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini. Alipoulizwa kipi hasa kilichoisukuma Takukuru kuwakamata na hatimaye kutaka kuwafikisha mahakamani Malinzi na Mwesigwa, kiongozi huyo alisema, “…hayo mengine yatafahamika mahakamani. Mimi siyo m...