Posts

YANGA HAO MOROGORO LEO.

Image
Mabingwa wa soka nchini klabu ya Yanga, leo inaondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Morogoro, kwaajili ya kambi kujiandaa na mchezo wake wa robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Singida United. Kikosi cha Yanga kinaondoka na wachezaji wake wote isipokuwa wale waliopo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Taifa Stars ambayo inajindaa na mchezo wake wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya DR Congo kesho na watajiunga na timu baada ya mechi hiyo. Wachezaji wanne wa Yanga waliopo katika kambi ya timu ya taifa ni kipa Ramadhan Kabwili, mabeki Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondan pamoja na kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib. Wapinzani wa Yanga, Simba wamekuwa wakiweka kambi yao Morogoro mara kwa mara. Yanga itakuwa Morogoro hadi Jumamosi ya Machi 31 ambapo itaelekea Singida kucheza na Singida United Jumatatu April 1 kwenye uwanja wa Namfua. Baada ya mchezo huo Yanga inatarajiwa kurudi Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania tiketi ya hatua ya makundi ...

NIYONZIMA.Mashabiki msinihesabie kuanza kwenye kikosi cha kwanza

Image
LICHA ya kuanza mazoezi, kiungo mnyumbulifu wa Simba, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, ameibuka na kuweka bayana kwamba mashabiki wa timu hiyo wasimhesabie kuanza kucheza katika kikosi cha kwanza kwa sababu bado hajapona vizuri majeraha yake. Niyonzima aliyetua Simba mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga, hajawa na msimu mzuri baada ya kupata majeraha ambayo yamemuweka nje kwa zaidi ya miezi miwili ndani ya kikosi hicho kilichopo mikononi mwa Mfaransa, Pierre Lechantre. Kiungo huyo hivi karibuni alianza mazoezi ya kujifua ufukweni kabla ya kuhamia katika gym ambapo alifanya sambamba na wachezaji kadhaa wa Yanga, wakiwemo Thaban Kamusoko na Amissi Tambwe ikiwa ni njia ya kujiimarisha. Akizungumza na Championi Jumatatu, Mnyarwanda huyo ambaye ni baba wa watoto mapacha, alisema kuwa licha ya kuendelea na mazoezi mbalimbali lakini hali yake bado haijatengemaa na kuanza kukitumikia kikosi hicho kwenye michezo yake 10 iliyobakia ya Ligi Kuu Bara. “Unajua watu wanaongea sana bila ya kufaha...

WASIOKUWA NA VITAMBULISHO VYA UTAIFA HAWATARUHUSIWA KUTUMIA SIMU.

Image
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imebainisha kuwa haitakuwa rahisi kwa mtu yoyote raia wa Tanzania kumiliki simu kama hatakuwa na kitambulisho cha Taifa. Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA, Rose Mdami, alisema pamoja na mambo mengine kwa sasa mamlaka hiyo inaendelea na usajili wa wananchi katika mikoa 20 ya Tanzania Bara, huku kwa upande wa Zanzibar zoezi likiwa limekamilika. Akizungumzia maendeleo ya uandikishaji huo, Rose alisema kuwa NIDA inaendelea kusajili Mamlaka za Udhibiti wa mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA) kwa lengo la kusajili wanachama na wanufaika wote wa mifuko hiyo nchini. Mbali ya zoezi hilo, Rose alisema pia wanaendelea kulifanyia kazi ni usajili wa kampuni za simu kwa sababu wateja wote wapya wa kampuni zote watakaotaka kusajili laini mpya watalazimika kuwa na vitambulisho vya taifa. “Majaribio ya zoezi hilo yanafanyika katika mikoa sita, kwa Dar es Salaam ni Mliman City, hivyo wananchi wanaokwenda kusajili laini za simu kama hawana vitam...

MAGAZETINI LEO jumatatu tar 26/03/2018,,,Yanga yawateka Waethiopia kila kona.

Image

HABARI MPYA NDANI YA YANGA HII HAPA.

Image
Kikosi cha mabingwa watetezi Wa VPL,Kesho wanatarajia kuanza mazoezi ya kujifua kuelekea mechi yao ya FA. Yanga wanarejea Leo kambini tayari kwa mazoezi hayo ikiwa in siku 6 Kabla ya mechi hiyo itakayopigwa tarehe Mosi uwanja Wa Namfua mjini Singida. Yanga itawakosa Kabwili,Yondani,Ajibu na Michael ambao wanaitumikia timu ya taifa Taifa Stars inayojiandaa na mechi dhidi ya Congo. Usisahau kutupa maoni yako.

WEMA AZUA GUMZO MITANDAONI BAADA YA KUACHIA MSAMBWANDA NJE NJE.

Image
MSANII wa Bongo Movies, Wema Sepetu amezua gumzo baada ya kuachia msambwanda wake LIVE wakati akiogelea pamoja na kaka yake Diamond Platnumz, Rommy Jones.  Katika kipande cha video kinachosambaa kwa kasi mitandaoni kinamuonesha Wema akikata mauno wakati wimbo wa Zaiidi wa Wowowo ukipigwa wimbo ambao unaonyesha kumfuyrahisha mlimbwende huyo na kuamua wowowo lake hadharani.

MAGAZETINI LEO TAR 25/03/2018.

Image
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MARCH 25,2018   Erick Picson     20 mins ago     Magazeti,