Posts

MAGAZETINI LEO 27/12/2017

Image

Yanga yaifunga mdomo Simba

Image
Ushindi wa Yanga wa mabao mawili 2-0 dhidi ya Reha FC imedhihirisha kuwa timu hiyo iliingia uwanjani ikiwa na ari ya kupata ushindi. Timu hiyo ya Jangwani ilifanya mashambulizi kadhaa ambayo wapinzani wao walijitahidi kufanya hivyo pia, lakini umakini wa makipa wa pande zote uliwafanya kuingia kipindi cha pili kwa kila timu bila kuona lango la mwenzake. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru umedhihirisha kuwa timu za Ligi Daraja la Pili siyo za kubeza kutokana na kuonyesha soka la kuvutia. Wiki hii Simba ambao walikuwa mabingwa mtetezi, walifungwa na Green Warriors timu ya Ligi Daraja la Pili mchezo ulioisha kwa kupigiana mikwaju ya penalti 4-3. Yanga imefanikiwa kuvuka hatua raundi ya tatu ya michuano hiyo ya Kombe la FA kwa mabao yaliyowekwa wavuni na Amissi Tambwe na Pius Buswita

MADHARA YA KUNYONYA AU KULAMBA CHUMVINI

Image
Wahenga washasema kila kizuri kina kasoro zake! Hili linajithibithisha baada ya mitindo hii ya mapenzi inavyoambatana na athari na madhara kedekede yakiwemo maradhi ya kuambukiza na magonjwa ya zinaa kwa wale wenye kuwa nayo! Duuh! Haya basi hii ni orodha ya magonjwa ya zinaa ambayo huambukizwa kupitia kulambana na kunyonyana  Sehemu Siri:- 1. Gonorrhea Hili huanzia katika koo la muambukizwaji, na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifuu au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadae hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi 2.  Syphilis Huu huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdoma na hasa pale inapotekea mdomo ukutana na kiungo chenye athari hizo.  3. Chlamydia Huu pia huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalali kwa muda mrefu 4.hepatitis A Huyu ni Virus anayepatikana katika kinyesi cha binadamu, huyu huwaingia wale wanaopenda kunyonyana na kulambana sehemu za haja kubwa 5.Hepatitis B Huu huambukizwa kama HIV vile maana virusi...

Tabia Ya Kuzoeana inavyoweza kuathiri Maisha yako ya kimahusiano

Image
  kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla. Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini. Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hi...

MAGAZETINI LEO 26/12/2017

Image

Barnaba Classic Atangaza Kuachana na Mziki

Image
Ikiwa zimebaki siku sita tu kabla ya kuumaliza mwaka 2017 na kuingia 2018, staa wa Bongofleva Barnaba Classic ametangaza kuwaaga mashabiki wake kwa mwaka huu na atakuwa kimya kimziki kwa muda. Mkali huyo wa sauti na uandishi kwenye kiwanda cha mziki Bongo, ameweka wazi kuwa ukimya wake utaanzia kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kujipanga namna ya kuuanza kwa kishindo mwaka 2018. “Nikiwa najitoa kwenye mitandao ya kijamii kidogo, ningependa kuwatakia mashabiki, marafiki na familia yangu Heri ya Christmas na Mwaka Mpya”, amefunguka Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram. Pamoja na kujitoa kwake nyota huyo anayetemba na ngoma yake ya Mapenzi Jeneza ameongeza kuwa anajiweka vizuri kuanzia mwonekano mpaka sound ya hit zake zijazo. “Ninapumzika kidogo ili kuweka mipango yangu vizuri kwaajili ya mwaka 2018. Nitawaletea Barnaba mpya mwenye kila jipya kimuziki na hata Sound” ameongeza

Hizi Ndizo Rekodi za Omog Simba

Image
LICHA ya kocha Joseph Omog raia wa Cameroon kutimuliwa ndani ya kikosi hicho, lakini takwimu zinaonyesha kuwa ipo kazi kwa mrithi wake kufanya kwa ajili ya kuzipiku takwimu ambazo ameziacha kwenye muda wa mwaka mmoja na miezi sita aliodumu kwenye kikosi hicho. Omog alifungashiwa virago vyake juzi Jumamosi baada ya kikao baina ya pande hizo mbili yaani uongozi wa Simba pamoja na Omog mwenyewe ambapo wote walikubaliana juu ya kusitishwa kwa mkataba wa kocha huyo ambao ulikuwa unaenda hadi tamati ya ligi msimu huu mwezi Mei. Licha ya kutimuliwa huko lakini kocha huyo atakumbukwa kutokana na kuirejesha timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa ambayo kwa misimu minne hawakushiriki baada ya kutwaa ubingwa wa FA walioutwaa msimu uliopita kwa kuwafunga Mbao FC ya Mwanza. Lakini pia Omog ilibaki kidogo aifikie rekodi ya kocha Patrick Phiri ya kucheza msimu mzima bila ya kuruhusu kupoteza pointi ambapo yeye kwenye msimu mzima alipoteza mechi nne pekee huku akishinda 21 kwenye mechi 30 za msim...