Posts

LEO KAMA JANA AU LAA. Tshishimbi kung'ara tena au laa

Image
Leo ni leo pia ambapo mabingwa watetezi YANGA watakuwa uwanjani, kuwavaa Wana wa Paluhengo LIPULI FC kutoka IRINGA huku yanga wakiwa na kiu kubwa tena mara baada ya kupewa kiu na watani wao wa jadi hapo Jana SIMBA mara baada ya kuwacharaza vilivyo RUVU katika uwanja wa Taifa.   Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa mnamo majira ya saa 10 jioni kulingana na ratiba, hivyo tupende kuwataarifu wapenzi wasomaji na watazamaji wa soka kuwa leo tutakuwa tukiwaletea matokeo yote live, kwa kutumia video za magoli nakadharika.  Dont miss it  By Godfrey Mpagike 

VIDEO: The best dancer in the world

Image

YANGA YAZIDI KUJIIMARISHA. Hatimaye Kiungo mpya asaini miaka Mwili

Image
HATIMAYE  kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), leo amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wa Tanzania, Yanga SC.  Mchezaji huyo alikuwa nchini wiki iliyopita kwa ajili ya vipimo vya afya na baada ya kufaulu akaambiwa afuate barua ya kuruhusiwa na klabu yake, Mbabane Swallows ya Swaziland kuondoka ili aje kusaini mkataba.  Baada ya kukamilisha taratibu hizo, Tshishimbi leo amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika mabao ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.  Na baada ya kusaini mkataba huo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye inaaminika ndiye mrithi wa Mnyarwanda, Haruna Niyonzima aliyekwenda kwa mahasimu Simba, anatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda kisiwani Pemba kuungana na kikosi cha Yanga kwa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Agosti 23.  Yanga ilivutiwa na Tshishimbi baada ya kumuona akiichezea ...

Msuva azidi kuwa vizuri (mechi 4 magoli 6)

Image
WINGA  wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefikisha mabao sita ya kufunga tangu amejiunga na Difaa Hassani El-Jadida (DHJ) ya Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola.  Hiyo inafuatia Msuva jana kufunga bao moja katika mechi yake nane DHJ ikifungwa 2-1 na timu ya Daraja la Kwanza, Union Sportive Musulmane Oujda (USMO) Uwanja wa El Abdi mjini Jadida.  “Jana nimefunga tena, hilo ni bao langu la sita sasa katika mechi nane zote za kirafiki. Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na hapa kila siku ninachojua ni bidii tu ili nitimize malengo yangu,”amesema Msuva akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo.  Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na DHJ Julai 28, mwaka huu baada ya kucheza  Yanga ya nyumbani, Tanzania tangu mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro.  Awali ya hapo, Msuva alipitia akademi ya Azam akitokea kituo cha kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi, Wakat...

NIYONZIMA awapa YANGA siri hii

Image
KIUNGO mpya wa kimataifa wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amewafichulia wapinzani wao wote wa Ligi Kuu Bara mambo ya ndani kuhusu kiwango chao akiwataka kujipanga vilivyo kuelekea ligi hiyo hapo Agosti 26, mwaka huu.  Akizungumza na gazeti hili jana, Niyonzima alisema kiwango walichoonyesha katika mechi dhidi ya Rayon ni sehemu ndogo ya "ufundi" walionao wachezaji wa timu hiyo ambao msimu ujao wamejipanga kuipa klabu yao mataji. Kiungo huyo aliyetua Simba hivi karibuni kwa kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, alisema kila mchezaji aliyesajiliwa Simba anafahamu kiu ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambao wamekosa ubingwa kwa miaka minne.  Niyonzima alisema kuwa kwa sasa wanaendelea kujifua na kabla ligi haijaanza, watakuwa wameimarika zaidi kwa sababu wachezaji wote wamekamilika na wanafanya mazoezi ya pamoja.  "Tutakuwa wazuri zaidi ligi itakapoanza, tulionyesha kiasi kidogo tu cha uwezo wetu, naamini masha...

MBILI KALI ZA YANGA LEO

Image
YANGA LEO  JUMAMOSI 12.8.2017 Mchezo wa Kirafiki Klabu ya Yanga Leo inatarajiwa Kushuka Dimbani Kucheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Chamazi katika Hali ya Kujiandaa na Ligi KUU Tanzania Bara na Mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Simba. Mchezo huo awali  ndugu mwana kwataunit.com ulikuwa uchezwe Taifa Ila Jana ulihamishiwa Chamazi Baada ya Yanga kupewa Taarifa kutoka Serikalini Kutoutumia uwanja huo. Yanga Itawakosa wachezaji wanne Yanga katika Mchezo wa Leo dhidi ya Ruvu itawakosa wachezaji Youthe Rostand, Beno Kakolanya, Mwashiuya na Obrey Chirwa wachezaji hawa wote ni majeruhi japo ndugu msomaji wa GODYNEWSTZ  hali zao zinaelezwa kuwa siyo mbaya sana. Kwamujibu wa Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema Afya zao zinaendelea Vizuri na wote wataungana kambi ya Pemba kujiandaa na Ligi na Mechi dhidi ya Simba

HUJACHELEWA MAGAZETI YA LEO 12/08/2017 HAYA HAPA

Image