MANULA:Ndo basi tena simba

Kipa wa Azam, Aishi Manula. WAKATI wachezaji wenzake wakitarajiwa kutambulishwa kwenye sherehe za Simba Day, kipa Aishi Manula atakosa fursa hiyo ndani ya kikosi cha Simba. Klabu ya Simba imekuwa na kawaida ya kuandaa tamasha mara moja kila mwaka ambapo huwa ni maalum kwa kukaribisha msimu husika ikiwemo kutambulisha wachezaji wao. Taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa kutoka kwa bosi mkubwa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na klabu yake ya Azam FC ni kuwa mkataba wa Manula unamalizika rasmi Agosti 10, mwaka huu huku dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa Agosti 6, mwaka huu. Imeelezwa kuwa kutokana na mkataba huo kumbana kipa huyo, itakuwa ngumu kwa Simba kukamilisha mchakato wa kumsajili bila kumalizana na Azam FC kwa kuwa ili asajiliwe lazima mkataba wake ndani ya Azam uvunjwe. “Mkataba wa Manula unatarajiwa kumalizika Agosti 10, mwaka huu, kwa maana hiyo kipa huyo hatakuwepo kwenye orodha ya wachezaji wapya watakaotambulishwa katika Simba Day....