MWISHO WA KUNUNUA TIKETI MECHI SIMBA NA YANGA.

Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mwisho wa kununua tiketi za mechi hiyo ni Ijumaa.

Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema mashabiki wenye nia ya kushuhudia mechi hiyo wawahi kununua tiketi mapema kabla ya siku hiyo kwakua siku ya mchezo hakutakuwa na zoezi hilo.

"Ijumaa ndio mwisho wa kuuza tiketi kwahiyo kama kuna mtu anataka kushuhudia mchezo huo moja kwa moja anapaswa kununua siku moja kabla. Siku ya Jumamosi hakutakuwa na muda wa kuuza tiketi," alisema Lucas.

Lucas amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa kinacho subiriwa ni muda kufika.

Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru ambapo viingilio ni sh 20,000 kwa jukwaa kuu na 10,000 kwa mzunguko

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).