MSUVA. Kuacha utoto ndio kilicho mtoa YANGA.

Image result for msuva

Kiungo mshambuliaji wa Mbao FC James Msuva amesema utoto ndio uliomfanya akaondoka ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kupandishwa kutoka timu ya vijana (U20) na aliyekuwa kocha wa Yanga wakati huo Hans van Pluijm.
“Ilikuwa ni utoto tu, baada ya kupandishwa kwenye timu ya wakubwa kuna siku tulikuwa na mechi ya kirafiki Yanga vs KMC, nikachelewa kufika. Tangu hapo mzungu (Hans van Pluijm) hakunielewa akanisimamisha nikabaki nyumbani.”
“Ilikuwa ni kipindi cha mwishoni mwa ligi, baada ya ligi kumalizika brother (Simon Msuva) akanishauri niende kujaribu sehemu nyingine nikaenda kujiunga na JKT Ruvu badae ikashuka daraja, sasa hivi nipo Mbao bado napambana.”
“Katika vitu ambavyo Msuva huwa ananishauri ni kujituma, anataka  nipambane mwenyewe watu waone ili wasiseme labda natumia jina lake. Mambo mengine huwa naona mwenyewe, kama changamoto na mafanikio anayopata.”
Alivyopandishwa kikosi cha wakubwa Yanga
Msuva amesema, walikuwa wakifanya mazoezi na kikosi cha wakubwa cha Yanga wakati wachezaji wa kikosi hicho walipokuwa wanaitwa kwenye timu ya taifa.
“Mwalimu alikuwa anatuchukua mimi na wenzangu wanne kwenda kuongeza idadi kwenye timu ya wakubwa wakati wachezaji wengine walipokuwa wanaitwa kwenye timu zao za taifa. Tulikuwa tunajaza nafasi za wachezaji walioondoka kwenda timu za taifa. Nikawa nafanya vizuri kwenye mazoezi mwalimu akanipandisha timu ya wakubwa.”
Changamoto ndani ya Mbao
“Mbao ni timu yenye vijana wengi, hapa kuna changamoto kubwa ya kupata nafasi kucheza. Kila mmoja anapambana kupata nafasi ya kucheza, naamini kupitia Mbao nitafanya vizuri na kufika juu ninapotaka mimi ikiwa ni pamoja na kucheza nje ya nchi. Kikubwa ni kuomba uzima na afya, hayo mengine yanawezekana kwa nguvu za Mungu.”
Ukimwambia amshauri Simon Msuva  
“Tunapokuwa tumekaa huwa namwambia kwamba ninamuamini, anachotakiwa kufanya ni kuongeza bidii zaidi ili kufikia malengo. Mwanzo alikuwa anapambana kutoka Tanzania kwenda nje, sasa hivi yupo nje ya Tanzania kwa hiyo bado kuna kazi ya kuhakikisha anatoka Afrika kwenda Ulaya au sehemu nyingine.”

Comments

Popular posts from this blog

Kubemenda Mtoto

Siwezi pitisha siku bila kutembea na malaya

HAYA NDIO MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KWA NJIA YA MDOMO. (Oral sex).