Posts

Showing posts from October, 2017

SIMBA KUSHINDWA KUWAFURAHISHA MASHABIKI WAO KIDATO CHA NNE TANGU FORM ONE.

Image
Habari za wakati huu ndugu msomaji wa blog yetu na mtazamaji wa online tv yetu iitwayo GODYNEWSTZ TV Ikiwa kama youtube channel. Leo katika pitapita kwenye mitandao ya kijamii ni matani nikakutana na utani wa kimichezo unaoendelea kunako mitandao hiyo ambao kama ni kuongeza siku za kuishi kwa kucheka kweli watu wameongeza siku zakuishi.  UTANI wenyewe ni kuhusu mabingwa mara 18 tangu mwaka ligi kuu tanzania bara ianzishwe. Unapenda kujua mautani hayo yakuvutia kwa leo ulikuwa kama hivi. Ni pale KLABU YA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA KUSHINDWA KUWAPA HAKI YAO MASHABIKI WAO WA FORM FOUR TANGU WAANZE KIDATO CHA KWANZA HAWAJASHUHUDIA KLABU YAO IKITWAA UBINGWA LIGI KUU VODACOM.  BY Godfrey Mpagike @kiraka. Usisahau kutembelea youtube channel yetu kupata habari mbalimbali kwa video. 

Mechi ya Simba na Yanga Leo ni Vita na Kisasi Uwanja wa Taifa

Image
MECHI za Ligi Kuu Bara z i n a t a r a j i a kuendelea wikiendi hii kwa mzunguko wa nane kuchezwa, huku miamba miwili ya soka Tanzania, Simba na Yan­ga ikitarajia kukutana kwenye Uwanja wa Uhu­ru jijini Dar es Salaam, kesho Jumamosi. Mchezo huu unatara­jiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hizo kuwa katika nafasi sawa ya msimamo wa ligi licha ya Simba kuongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga, huku kila moja ikihitaji kukaa kileleni. Mechi hii inatarajiwa kuwa ni ya vita na kisasi kutokana na hali jinsi ilivyo katika mechi husika ambapo kila upande utahitaji ku­fanya vyema. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatarajiwa kuifanya mechi hiyo kuwa ni ya vita na kisasi. MAKOCHA KUTETEA VIBARUA VYAO Imekaa vibaya kwa upande wa makocha wa timu zote mbili, kutokana na historia za timu hizo ambapo mara nyingi makocha wamekuwa wakifungashiwa vi­rago vyao pale wanapofungwa na wapinzani wao. Hivi karibuni kulizuka uzushi juu ya Yanga kutaka kumuondoa ko­cha wake, George Lwand...

TCU YATANGAZA MWISHO WA KURIPOTI WANAFUNZI WAPYA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Image
Wanafunzi ambao tayari wamekidhi vigezo na kupitishwa kujiunga na elimu ya juu wanatakiwa kuripoti chuoni ili kuanza masomo ifikapo Oktoba 30, amesema hayo leo kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Eleuther Mwageni . Prof. Mwageni ameyasema hayo leo wakati anatoa ufafanuzi juu ya tarehe ya kufunguliwa kwa vyuo kutokana na mkanganyiko ambao wameupata baadhi ya wanafunzi kuhusu muda sahihi wa masomo kuanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 hususani wale ambao wameomba nafasi kwenye awamu za pili na tatu za Udahili. “Tarehe ya Kalenda ya masomo haijabadilika iko palepale ambayo ni Oktoba 30 wanafunzi wanatakiwa kuanza masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018”, amesema Mwageni. Aidha Prof. Mwageni ameeleza kuwa zaidi ya wanafunzi 450,000 tayari wameshapata vyuo hivyo kinachosubiriwa katika awamu ya tatu ni kupitisha wanafunzi wengine 12,000 ili kufikia malengo ambayo ni wanafunzi 57,000. Awamu ya tatu ambayo ilianza Oktoba 18 hadi 22 imefikia hatua nzuri ambapo ...

MWISHO WA KUNUNUA TIKETI MECHI SIMBA NA YANGA.

Image
Zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mwisho wa kununua tiketi za mechi hiyo ni Ijumaa. Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema mashabiki wenye nia ya kushuhudia mechi hiyo wawahi kununua tiketi mapema kabla ya siku hiyo kwakua siku ya mchezo hakutakuwa na zoezi hilo. "Ijumaa ndio mwisho wa kuuza tiketi kwahiyo kama kuna mtu anataka kushuhudia mchezo huo moja kwa moja anapaswa kununua siku moja kabla. Siku ya Jumamosi hakutakuwa na muda wa kuuza tiketi," alisema Lucas. Lucas amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa kinacho subiriwa ni muda kufika. Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Uhuru ambapo viingilio ni sh 20,000 kwa jukwaa kuu na 10,000 kwa mzunguko

Bilionea IPTL apelekwa Muhimbili

Image
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetekeleza amri za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kumpeleka mshtakiwa katika  kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo. Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai leo Ijumaa amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa wametekeleza amri za Mahakama walizopewa kwa kumpeleka Sethi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari. Swai ameeleza kutokana na hali hiyo, Sethi atarudishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuchukua majibu ya vipimo vyake wiki ijayo. Baada ya maelezo hayo wakili wa mshtakiwa, James Rugemalira, Respicius Didas ameeleza mahakamani hapo kuwa kuna suala la ucheleweshwaji wa upelelezi na kwamba washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Juni 19,mwaka 2017 na wapo ndani hadi sasa. Wakili Didas ameeleza kuwa upande wa mashtaka unawaambia upelelezi bado hau...

MAGAZETINI LEO.

Image

OKWI Aizuga YANGA

Image
MKALI wa mabao wa Ligi Kuu Bara, Emmanuel Okwi wa Simba, ameizuga Yanga kwa kusema kwa sasa anaiwaza zaidi mechi yao ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar kuliko mchezo wao na Yanga. Simba wikiendi ijayo itacheza na Mtibwa mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, halafu itavaana na Njombe Mji Oktoba 21, kabla ya Oktoba 28, mwaka huu kucheza na Yanga katika ligi hiyo. Okwi, raia wa Uganda, ndiye anayeongoza kwa ufungaji katika ligi hiyo akiwa na mabao sita akifuatiwa na Mohammed Rashid wa Prisons mwenye mabao manne. Pia Habib Haji wa Mbao FC na Shiza Kichuya wa Simba nao wana mabao matatu kila mmoja. “Najua Yanga ni timu kubwa na ndiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu, ila ukiangalia msimamo wa ligi kuu ulivyo kwa sasa nalazimika zaidi kuitazama Mtibwa ambayo ndiyo tutacheza nayo kabla ya Yanga. “Mtibwa imekuwa na matokeo mazuri, hivyo nina kila sababu ya kuiwazia hiyo na baada ya mchezo huo na matokeo yake ndiyo yatanifanya kuifikiria tena Yanga jinsi gani tutapa...

MANARA:YANGA mnacheza na NJUGUMAWE AU.

Image
hajismanara Follow 1,411  likes 264  comments Nchi ya ajabu sana hii!!ikicheza Simba,game kama hz mnasema twacheza ndondo!!sasa nyie mnacheza nn;okey,mnacheza Njugumawe au kunde,,,Shubamit!!