Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteua madiwani nane wa Viti maalum wa CCM na CHADEMA kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika halmashauri nane za Tanzania bara, ambapo CCM yenyewe imefanikiwa kupata nafasi tano huku tatu zikienda CHADEMA. Hayo yamewekwa wazi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Julai 21, 2018 na kusema uteuzi huo umefanyika baada kukaa kikao cha tume hiyo cha Julai 19, 2018. Walioteuliwa ni Ajila Kalinga (CCM-Songea), Mary Kazindogo Mbilinyi (CCM Makete), Zainab Abdu Mabrouk (CCM-Kongwa), Restuta Aloyce Gardian (CCM-Muleba), Siglinda Silvester Ngwega (CCM-Morogoro). Wengine ni Zena Said Luzwilo (CCM-mji Kahama), Neema Michael Massawe (Chadema Monduli) na Teodola Muyula Kalungwana (Chadema-Iringa). "Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa aliitarifu tume ya uchaguzi kuwepo kwa nafasi hizo wazi ...