Posts

Showing posts from July, 2018

NEC yafanya uteuzi, CCM yaramba dume

Image
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteua madiwani nane wa Viti maalum wa CCM na CHADEMA kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika halmashauri nane za Tanzania bara, ambapo CCM yenyewe imefanikiwa kupata nafasi tano huku tatu zikienda CHADEMA. Hayo yamewekwa wazi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Julai 21, 2018 na kusema uteuzi huo umefanyika baada kukaa kikao cha tume hiyo cha Julai 19, 2018. Walioteuliwa ni Ajila Kalinga (CCM-Songea), Mary Kazindogo Mbilinyi (CCM Makete), Zainab Abdu Mabrouk (CCM-Kongwa), Restuta Aloyce Gardian (CCM-Muleba), Siglinda Silvester Ngwega (CCM-Morogoro). Wengine ni Zena Said Luzwilo (CCM-mji Kahama), Neema Michael Massawe (Chadema Monduli) na Teodola Muyula Kalungwana (Chadema-Iringa). "Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa aliitarifu tume ya uchaguzi kuwepo kwa nafasi hizo wazi ...

Yanga Yaleta Kiungo Kutoka Afrika Kusini

Image
   AKILI za viongozi wa Yanga zinaonekana hazipo tena kwenye Kombe la Shirikisho inayoendelea, kwani jana wachezaji waligoma lakini kuna kiungo kutoka Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Kingsley ametua kusajiliwa. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo irejee nchini ikitokea Kenya ilipokwenda kucheza na Gor Mahia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Yanga walifungwa mabao 4-0. Jana wachezaji waligoma kufanya mazoezi wakishinikiza wapewe chao lakini viongozi wanaonekana kuangalia zaidi msimu ujao. Yanga tayari imesajili wachezaji sita hadi hivi sasa ambao ni Mohamed Issa ‘Banka’, Mrisho Ngassa, Deus Kaseke, Jaffary Mohamed, Heritier Makambo na Fei Toto . Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongoman, Mwinyi Zahera alisema kiungo huyo alitua hivi karibuni kwa siri nchini akitokea Sauzi alipokuwa akicheza soka kabla ya kukabidhiwa na kuanza majaribio. “Bado viongozi wanaendelea na usajili wao na kama unafahamu tayari nimewashauri viongozi wasajili wacheza...

UMEIPATA HII KUHUSU GIGY MONEY.

Image
Video vixen Gigy na muimbaji Gigy Money amesema kwa sasa yupo pamoja na baba mtoto wake Mo Jay ikiwa ni miezi kadhaa toka wagombane na kurushiana maneno ya kashfa kupitia mitandao ya kijamii. Gigy amesema kwa sasa yupo tayari hata kumzalia watoto kwa kuwa amegundua mtangazaji huyo wa Choice FM ni mwanaume makini

KWELIIIIII!!!!!! NAMNA UNAVYOWEZA KUACHANA NA MCHEPUKO NA KUBAKI NJIABKUU.

Image
Habari za muda huu rafiki yangu, bila shaka u mzima na unaendelea na utaraitibu wako wa kila siku wa kutafuta griss ili kulaini vile vyuma vilivyokaza. Na siku ya leo naomba tujifunze kwa pamoja kuhusu ni kwa namna gani tunaweza kuachana na michepuko, kwani nimekuwa nikipokea jumbe nyingi sana za wasomaji wangu,  wengi wakiniuliza afisa mipango nifanye nini ili niweze kuachana na mchepuka na kubaki njia kuu? Nami bila hiana naomba nitirike hapa siku ya leo ili niwaponye wengi kwani swali la aina hii limekuwa likiwatesa wengi,  kwa sababu wengi wa wanaume au wanawake ambao wanachepuka imekuwa ni suala gumu sana kuweza kuondoka katika mchepuko na kubaki njia kuu. Mtego ambao umekuwa unatumiwa na michepuko kuwanasa wapenzi wa watu wengine, umekuwa upo vizuri kwa sababu pindi watu wanasapo imekuwa ni ngumu sana kunasuka. Kama na wewe ni miongoni mwa watu hao ambao wamekuwa wakichepuka na wameshindwa kunasuka unachotakiwa kufanya ni; 1. Unapokuwa upo pamoja na mchepuko au wahenga...